Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Wednesday, August 22, 2012

TUNDU LISU ALIPUKA


Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Monday, August 13, 2012

MNYIKA AKANUSHA MADAI YA CCM


Katika mitandao ya kijamii kumesambazwa habari zikimnukuu msemaji wa CCM kutoa madai mbalimbali ya uzushi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea kutekeleza mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini. Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa kwa ukamilifu, hata hivyo kuhusu madai yaliyokwisha sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM nachukua fursa hii kutoa kauli ya awali kama ifuatavyo:

Wednesday, August 1, 2012

UKWELI UNAFICHWA TUHUMA ZA RUSHWA BUNGENI - CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimelaumu juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Wednesday, July 11, 2012

DKT.SLAA ASEMA LIWALO NA LIWE HAWEZI KUHOJIWA NA POLISI


Katibu Mkuu wa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Willibrod Slaa amesema hawezi kujipeleka polisi kuhojiwa kutokana na kauli yake kwamba yeye na viongozi wengine wawili wa chama hicho wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa, huku akieleza sababu mbili za kugomea wito huo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.Juzi, Dk Nchimbi aliliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi wote wa Chadema waliotoa tuhuma za kutaka kuuawa hata kama wao hawana imani na jeshi hilo.

Tuesday, July 10, 2012

WABUNGE JADILINI HOJA; MNACHUKIZA WANANCHI KWA VIJEMBE MNAVYOTOA



Spika wa Bunge, Anne Makinda.
TUKIWA katika hali ya kutafakari amani ya nchi hii, tumshukuru Mungu kwani bado anatupenda na tuzidi kumuomba ili atuepushie na mifarakano yoyote ambayo inaweza kugawa taifa letu.
Baada ya kusema hayo nizungumzie bunge letu tukufu linaloendelea kuketi mjini Dodoma katika kikao cha bajeti ya serikali.

Thursday, July 5, 2012

MUUNGANO WAIBUI HOJA NZITO BUNGENI

*Upinzani wataka historia yake iwekwe hadharani *Wadai itasaidia kuwaondoa hofu Watanzania wote

KAMBI ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema historia halisi ya Muungano uliopo, imekuwa ikifichwa licha ya ahadi za mara kwa mara juu ya elimu itakayotolewa kwa umma kuhusu jambo hilo.

Wednesday, July 4, 2012

MVUTANO BUNGENI CCM, CHADEMA, CUF

'liwalo na liwe' *Mhagama apata wakati mgumu kutuliza malumbano bungeni *Nchemba ahusishwa na ufisadi, Mnyika atakiwa kuthibitisha

HALI si shwali ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndivyo tunavyoweza kusema kutokana na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), kurushiana makombora mazito.

Monday, June 25, 2012

SIASA ZA UDINI CCM ZITAIGAWA NCHI

Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Philemon Ndesamburo, amesema misingi mibovu ya siasa za udini iliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), itaigawa nchi na kuleta machafuko.

CUF WATAKA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ICHUNGUZWE

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kauli aliyotoa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, kuwa atavifuta baadhi ya vyama vya mifukoni, inaudhi na kusikitisha hivyo ofisi yake inapaswa kuchunguzwa.

Saturday, June 23, 2012

WASHIKA MPINI MNAWAHISHA MAZISHI YA CCM KABLA YA 2015


 BADO najiuliza kwa nini “washika mipini” (Spika, Majaji, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri, n.k) kwa maksudi wanachukua maamuzi ya kusiliba kaburi la ccm? Hakuna hata mmoja anajifunza kutokana na makosa yake ya awali au ya mtangulizi wake!

Friday, June 22, 2012

MBOWE:90% YA WABUNGE WAMETUMIA RUSHWA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amesema aslimia 90 ya wabunge wote wametumia wametumia rushwa kuingia madarakani

Alisema kitendo cha Mbunge wa Bahi mkoani Dodoma Bw. Omari Badwel kukamatwa na rushwa hakihitaji mjadala mpana kwani huo ni utamaduni wa kawaida kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Thursday, June 21, 2012

SPIKA AWAPA ONYO WABUNGE



Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda jana aliwataka wabunge kujadili bajeti ya serikali kwa uadilifu badala ya kutumia lugha ya matusi na kuanzisha malumbano yasiyo na tija. Bi Makinda aliyasema hayo bunge mjini Dodoma baada ya kumaliza kipindi cha maswali na kusisitiza kuwa, baadhi ya wabunge wamekuwa wakitoa michango isiyohusiana na bajeti.

Wednesday, June 20, 2012

MEMBE AKANUSHA UVUMI WA KUTABILI USHINDI CHADEMA

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard  Membe amewatupia kombora rafiki zake wa karibu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio ameanzisha kwa kutabili ushindi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salam jana, Membe alisema kuwa,kuna uvumi uliotokea wakati yeye akiwa safarini kuwa amekitabiria chama cha CHADEMA kuwa mshindi  ifikikapo   mwaka 2015.

MBATIA AIRUSHIA KOMBORA TAASISI YA AGHA KHAN



Mbunge wa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, James Mbatia ameitupia kombora Taasisi ya Agha Khan kutokana na kupewa misahama ya kodi tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961.Mbatia alitoa kauli hiyo jana bunge alipokua akichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya 2012/13,ambapo alisema ili taifa liendelee ni lazima liangalie misamaha ya holela ya kodi zinazotolewa kwa taasisi binafsi

WANANCHI WANATAKA ZAHANATI

MBUNGE wa jimbo la Kibondo Mkoani Kigoma Bw.Felix Mkosamali ameiita Serikali inayoongozwa na chama chama Mapinduzi kuwa imepararaizi kutoka na kushindwa kuongoza nchi

Akichangia mjadala wa bajeti bungeni Mjini Dododma  Mbunge huyo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi alisema wananchi wanataka zahanati na si kuongeza mikoa mipya na wilaya mpya na kuongeza matumizi ya serikali kwa kununua magari aina ya vx kwa viongozi

MNYIKA AFUKUZWA BUNGENI BAADA YA KUKATAA KUFUTA KAULI

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli yake ya kuwa Raisi  wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu na Bunge ni zembe na Upuuzi wa CCM ndivyo vimechangia mambo kuwa mabaya hivi. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.