Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amesema aslimia 90 ya wabunge wote wametumia wametumia rushwa kuingia madarakani
Alisema kitendo cha Mbunge wa Bahi mkoani Dodoma Bw. Omari Badwel kukamatwa na rushwa hakihitaji mjadala mpana kwani huo ni utamaduni wa kawaida kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Bw.Mbowe aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na wandishi wa habari ,Alisema suala la rushwa limeonekana ni jambo la kawaida na ndio utamaduni wa CCM hasa katika chaguzi zao za ndani na Uchaguzi Mkuu
Akieleza sababu za CHADEMA kujitoa katika uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki, Bw. Mbowe alisema hali hiyo ilitokana na uchaguzi huo kutawaliwa na rushwa za nje nje
"Baada ya kuona hali hiyo, nilimweleza Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, kuwa mfumo huu wa rushwa hadi kwenye uchaguzi wa Afrika Mashariki unalitia aibu taifa
"Nimekuwa nikikemea rushwa tangu kwenye vikao vya kamati ya Uongozi wa Bunge inayoongozwa na Spika, Bi.Anne Makinda, hadi sasa hakuna tamko lolote ambalo limetolewa kutokana na vitendo hivyo ambavyo vimegeuka kuwa utamaduni ndani ya CCM
"Asilimia kubwa ya wabunge wwamejaa fikra za rushwa si Bw. Badwel pekee, wabunge wetu asilimia 90 wameingia madarakani kwa rushwa na hili pia nilimueleza Dkt. Bilal kuwa wabunge wanahongwa je wananchi wa kawaida itakuaje" alisema
Akizungumzia madai ya chama hicho kupokea fedha kutoka nchi za Magharibi kwa lengo la kuziwezesha nchi hizo kuchota rasilimali nchini Mbowe alisema CHADEMA hakijapokea fedha zozote kutoka kwa mataifa hayo
Pamoja na hayo Bw. Mbowe alizungumzia suala la ushoga, mahusiano ya CHADEMA na chama cha Conservative nchini Uingereza ambacho kinaunga mkono sera ya ushoga
Alisema kabla ya waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. David Cameron hajaingia madarakani chama hicho kilikuwa na mahusiano na chama chake na kusisitiza kuwa sera za kukubali ndoa za jinsia moja zilipitishwa wakati wa utawala wa Waziri Mkuu, Bw. Tonny Blair wa chama cha Labour ambacho kina urafiki nha CCM
"Swala la ushoga ni swala la vyama vya siasa nchini Uingereza, kuwa rafiki wa chama cha Conservative, hakumaanishi kuwa sisi tutaungana nao kwa kila wanachokitaka" alisema
No comments:
Post a Comment