Wednesday, June 20, 2012

WANANCHI WANATAKA ZAHANATI

MBUNGE wa jimbo la Kibondo Mkoani Kigoma Bw.Felix Mkosamali ameiita Serikali inayoongozwa na chama chama Mapinduzi kuwa imepararaizi kutoka na kushindwa kuongoza nchi

Akichangia mjadala wa bajeti bungeni Mjini Dododma  Mbunge huyo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi alisema wananchi wanataka zahanati na si kuongeza mikoa mipya na wilaya mpya na kuongeza matumizi ya serikali kwa kununua magari aina ya vx kwa viongozi


Alisema bajeti ya mwaka jana serikali ilishindwa kuitekeleza na vilevile bajeti ya mwaka huu nayo badala ya kuongezeka inashuka kuanzia mifugo uvuvi na uwindaji vimeshuka na badala ya kupanda imekuwa ikiendelea kushukua

"Wananchi wa Kibondo wamenituma nisiunge mkono hoja kwa kuwa Serikali hii imepararaizi kwa kutuletea takwimu za mwaka 2006 na sisi hatutawavumilia hata kidogo na mwaka 2015 tuongezeka humu bungeni ili tuwakomboe wananchi wa nchi hii

Alisema si kwamba wapinzani wamekuwa wakikamia lakini lazima waseme ukweli kwani hata kodi Serikali imeshindwa kukusanya makapini ya simu kama vodacom,tigo ,Air Tel hawalipi kodi sasa Serikali imeshindwa kukusanya kodi kuanzia ngazi ya kijiji hadi juu hii ndio maana wapinzania wanasema Serikali imeshindwa kuongoza nchi hii

Naye Bi. Nomi Keihula (CHADEMA ) alisema kazi ya wapinzania ni kuisimamia serikali na si kupinga kila kitu na tunaomba tuombewe wote humu ndani ili tuache kutoa misamaha ya kodi na tulikubaliana wabunge wote kuwa misamaha ya kodi hapana sasa iweje tena wenzetu wanageuka na kutoa misamaha ya kodi

Alisema Tanzania inajiuza yenyewe gesi imegundulika mataifa ya mengine yanapigana kuja hapa sasa ardhi na gesi ni yetu na wao wawekezaji wanakuja na mitambo sasa kinachotakiwa ni mikataba mizuri hivyo wanaccm wasichukie kwani kwa hilo hata baba wa Taifa alisema

No comments:

Post a Comment