Mbunge waa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alifukuzwa ndani ya ukumbi wa Bunge Jumanne Juni 19, 2012
Tuliona la Dr. Slaa na EPA Bungeni mwaka 2007, CDM wakashinda kesi Mahakam ya Wananchi na bado wanazidi kuvuna riba ya makosa yalitokana na udhaifu wa Bunge la wakati ule. Ikaja mwaka 2008 Zitto akafukuzwa Ubunge, wimbi la ushindi wa kuungwa mkono na wananchi likaendelea kusimama upande cha CDM. Bunge jipya 2011 tumewabeza CDM na Katiba, leo hii tunafakamia matapishi yetu tukiwa chooni kwa wapinzani. Juzi juzi tu Jaji wa Mahakama katika kesi ya Uchaguzi wa Arusha, kwa kufikiri amefanya kazi ya kusifiwa na chama, kaleta balaa uraiani kwa kumuacha Godbless Lema alande lande nchi nzima. Sasa badala ya watu wa Arusha wavue magamba, nchi nzima hata watoto wanavaa magwanda. Bado tu hatujajifunza wala kuwafunza au kuwaeleza watoa maamuzi kwamba; chonde chonde kujipendekeza kwenu kwa nia ya kuinusuru Chama Tawala, serikali na Taasisi zake (Bunge, Uraisi, Mahakam) havisaidii bali ndo vinamwaga petrol kwenye tanuru la kuni kavu za zinazoiteketeza serikali! Wananchi wa Tanzania ya leo, si wa Tanganyika ya Mwaka 1947! Wana maamuzi rohoni mwao tayari kwa kiama cha serikali yao hapo mwaka 2015.
Ukiyatazama haya yote huwezi kuja na uamamuzi kama wa leo juu ya JJ Mnyika. Watoa maamuzi wa serikali yetu ya ccm lazima wajue kuwa hawa CDM wakati mwingine wanachezea sharubu za simba maksudi kwa sababu wanajua Simba mwenyewe ni wa plastiki. Na akibahatika kuwa na betri yenye chaji inayomwezesha kuunguruma basi ni furaha zaidi Maana watoto wa wana CDM wanafaidi muungurumo wake!
Hivi kuna upya gani katika neno *“UDHAIFU”* lililosemwa na Mnyika leo Bungeni? Mbona watu wengi sana ikiwemo viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa wamelisema na kulirudia neno hili na wakilihusisha na Taasisi ile ile (Rais Kikwete) bila kuchukuliwa hatua yoyote?
Juzi Prof. Lipumba kasema wazi *Rais JK *ni *dhaifu* na kaenda mbali zaidi kumsifia Mkapa na utawala wake. Mh. Sitta akiwa Spika aliwahi kusema “kiutu uzima” kuwa *“wewe rais umekuwa mpole mno” *Hapa kwa wenye kung’amua Sitta alitumia uungwana tu kukwepa kutumia neno DHAIFU. Angeweza kusema *“wewe rais umekuwa DHAIFU mno*”. Pia mwandishi Kondo Tutindaga – katika MwanaHalisi ya tarehe 01 June 2011 iliyobeba kichwa cha mada “ Ni ubaya wa Lowassa au udhaifu wa JK?” alitumia neno “UDHAIFU” kama kisifa cha Rais JK si chini ya mara 15. Upya uko wapi mpaka huyo Spika anampa Mnyika kupiga penalti kwenye goli lisilo na golikipa?!
Hapa chini ni baadhi ya waandishi wachache tu miongoni mwa Watanzania lukuki walisema hadharani UDHAIFU wa Rais Kikwete
—Quote—
Kondo Tutindaga
………..Hali ya nchi kwa sasa ni tete kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Wale wanaojipendekeza kwa Rais Kikwete ni wepesi kumshauri kuwa anayesababisha haya ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na wengine wanamwambia sababu ni mapacha watatu. *Hakuna anayemwambia rais kuwa udhaifu wake ndicho chanzo cha utete wa taifa*…………
—End Quote—
—Quote—
Pasco
Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia *JK is a weak president,* watu hawataki kukubali!. Hao masheikh wa kukundi cha Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo wakakamatwa!. *Kwa huu udhaifu wa JK,* sasa sio tena CCM itamfia mikononi
—End Quote—
—Quote—
Kondo Tutindaga
….. Lakini upo upande wa pili unaowakilishwa na udhaifu wa Kikwete kama Rais na mwenyekiti wa chama chetu. Rais na *mwenyekiti mwenye udhaifu wa kiuongozi* husababisha makundi ya watu wanaojipendekeza kwake au kujituma kufanya mambo ambayo yeye angefanya……..
…….Kwamba, *udhaifu wa Kikwete* ambao wakati mwingine unaitwa “uungwana wake” kwa vile unatendwa na mkuu wa nchi, ndio unaosababisha makada wachinjane, wauane, wakamiane, wasingiziane, na hatimaye waangamizane kisiasa……..
*………Udhaifu wa Kikwete* umelifikisha taifa mahali pagumu sana. Ili kurekebisha hali hii, gharama kubwa kisiasa na kiuchumi itatumika. Rais kwa hofu na aibu ya kusemwa sana na watu, anaweza kuzinduka na kuchukua hatua kwa jazba na hasira na kufanya makosa yanayoweza kuligharimu taifa kwa muda mrefu……….
—End Quote—
—Quote—
*Saed Kubenea
MwanaHalisi 30 November 2011
Kikwete, Lowassa hapatoshi*
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, *Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM *kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.
—End Quote—
Imeandikwa na Omutwale wa JamiiForums
No comments:
Post a Comment