Showing posts with label Mtazamo. Show all posts
Showing posts with label Mtazamo. Show all posts

Saturday, August 11, 2012

MAKOSA YANAYOFANYWA NA MABINTI WAINGIAPO KWENYE MAHUSIANO


Makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua nani wa kumuoa ,kuolewa ni swala la makubaliano kati ya watu wawili wenye jinsia tofauti .Katika harakati za kuolewa kuna masuala mengi ya kuangalia ili binti asifanye kosa wakati wa kuchagua mtu wa kumuoa , kosa kwa binti anayetaka kuolewa ni kama ifuatazo

Kuamua kuolewa na mtu ambaye ni mkorofi , ukiwa na mayawo kuwa ataweza kubadilika akiwa ndani ya ndoa , ni vigumu sana mwanaume kuondoa dosari zake wakati akiwa ndani ya ndoa tena mbali na hiyo atazidisha dosari .Kama wewe unatarajia kuolewa hivi karibuni kuwa makini na neon ‘I LOVE YOU’ kuna wanasakolojia wanaeleza kuwa hilo neon maana yake ni ‘NINA UCHU NAWE’ kwani asilimia kubwa wanatamani mwili na hawana kitu kingine mbali na mapenzi

Friday, August 3, 2012

TUJITAHIDI KUONGEZA WASHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Kwa uchanganuzi uliofanywa na blog views, umeona kuwa Tanzania ingepaswa kuwa na washiriki zaidi ya Nchi jirani kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea Mjini London hivi sasa, kutokana na hali nzuri ya kisiasa na mahusiano yake kimataifa.

Monday, July 30, 2012

MTAZAMO KUHUSU MAFANIKIO


Kufanikiwa hakuitaji kuwa na sura nzuri na umbo lenye mvuto, unachopaswa ni kutumia akili yenye maarifa na uwezo wa kutekeleza mambo.

Friday, July 27, 2012

MNYIKA "TUTIBU KIINI CHA TATIZO SEKTA YA NISHATI YA UMEME


Kwa nafasi ya Uwaziri Kivuli wa Nishati na Madini,nafahamu kuna ufisadi na ubadhilifu ndani ya TANESCO ambao uchunguzi ni muhimu kwa ajili ya uwajibikaji.Kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa TANESCO na maafisa wengine wa shirika hilo kupisha uchunguzi ni muhimu,lakini si muarubaini wa uozo wa kimfumo katika sekta ya nishati nchini nitatoa vielelezo vya kina wakati nitakapo wasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni katika wizara ya Nishati na Madini.

Hata hivyo ni vyema nikatahadharisha mapema kuwa tukio hili linapaswa kutafakariwa kwa upana kwa kuwa linahusisha masuala mengi ambayo mengine Bodi ya Wakurugenzi imeyaacha nyuma ya pazia.Ukweli wote utakapotoka hadharani wengine zaidi watapaswa kuwajibika au kuwajibishwa kwa maslahi ya Taifa!

Monday, July 23, 2012

MWANAMKE ANAPOCHOKA KATIKA MAHUSIANO


Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.

Saturday, July 21, 2012

KITCHEN PARTIES HUIMARISHA NDOA AU KUIBOMOA


Mara nyingi hutumika kwa ajili ya mafundisho ya ndoa kwa mtoto wa kike anayetarajiwa kuolewa au kuishi na mume, Wanapewa mafunzo ya ndoa na mapenzi kwenye mikusanyiko inayoitwa "kitchen Parties".  Mwanafunzi huyo anatarajia kupata vingi vipya ikiwemo na viombo vya ndani hususani vya jikoni Katika mafunzo hayo wanaambiwa mambo ya mapenzi na hususan jinsi ya kufanya mambo fulani fulani na kuhusiana na mwenza. Matarajio ya mafundisho hayo ambayo hukusanya wanawake wengi ni kuwa mfundwa (kama tunaweza kuita huko ni kufundwa) ni kwamba atakuwa amejiandaa kwa maisha ya ndoa na mapenzi.

Wednesday, June 20, 2012

MAVAZI YANACHOCHEA MAHUSIANO KATIKA JAMII

Mavazi ni kitu pekee katika maisha ya mwanadamu ambayo kwa namna moja ama nyingine huongeza mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume hasa watu wanapokuwa katika uchumba kabla ya kuingia katika mahusiano ya ndoa kama mke na mume

Mwanaume naye huwa ana nafasi yake kwa mwanamke ambapo wanawake wa kisasa wanataka mvulana ambaye yupo (smart) msafi na mtu wa kupangilia nguo zake wakati anapotaka kutoka kwenda kazini ama siku ya kupumzika ambapo lazima uwe na mavazi ya siku ambazo huendi kazini

WATOTO WANANAFASI KUBWA KATIKA FAMILIA

WATOTO katika familia wana raha  pale tu wanapopata malezi bora kutoka kwa wazazi wao hasa wakiwepo wote wawili baba na mama

Wataalamu mbalimbali duniani wameorodhesha hatua kama nne katika makuzi mbalimbali ya mtoto ikiwemo ya mtoto kula chochote anachoshika mkononi,kujisaidia na kumpenda sana mzazi mmoja wapo ambapo anaweza kuwa baba ama mama