Thursday, June 21, 2012

SPIKA AWAPA ONYO WABUNGE



Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda jana aliwataka wabunge kujadili bajeti ya serikali kwa uadilifu badala ya kutumia lugha ya matusi na kuanzisha malumbano yasiyo na tija. Bi Makinda aliyasema hayo bunge mjini Dodoma baada ya kumaliza kipindi cha maswali na kusisitiza kuwa, baadhi ya wabunge wamekuwa wakitoa michango isiyohusiana na bajeti.

Aliwataka wabunge kutoa michango yao kwa kuielekeza bajeti hiyo pamoja na kuepuka malumbano yasiyo na tija kwa taifa na wanachi waliowachagua. “Wananchi wanatuma ujumbe mfupi wa simu kuuliza nini ambacho wabunge wanajadili mnakwenda nje ya bajeti siku zote huwa nawaambia kuwa wananchi wanaangalia tunachokifanya” alisema Bi. Makinda

Alisema mambo yanayoendela katika bunge hilo ni tofauti na kazi walizotumwa na wananchi wao. “Wabunge fanyeni kile mlichotumwa na wananchi wenu kumbukeni kila mnachozungumza wananchi wenu wanaona na wanahoji kama ndicho walichowatuma kuweni makini “ alisema Bi. Makinda na kuruhusu mjadara wa bunge kuanza

No comments:

Post a Comment