Wednesday, June 20, 2012

MEMBE AKANUSHA UVUMI WA KUTABILI USHINDI CHADEMA

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard  Membe amewatupia kombora rafiki zake wa karibu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio ameanzisha kwa kutabili ushindi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salam jana, Membe alisema kuwa,kuna uvumi uliotokea wakati yeye akiwa safarini kuwa amekitabiria chama cha CHADEMA kuwa mshindi  ifikikapo   mwaka 2015.


Alisema kuwa huo ni uvumi ambao hauna ukweli ndani yake na kama kuna mtanzania anadhani kuwa amesema hivyo basi ajitokeze ili ukweli ujulikane.

"Najua huo ni mkono wa mtu tu na nitapeleleza mimi ni mwana CCM na hichi kitu kimewekwa makusudi ili kunifitinisha naliwakaribisha vijana wa CHADEMA kwa ukarimu wangu tu na si mambo mengine kama watu wanavyonizushia"alisema Membe.

Aliongeza kuwa upinzani si uadui Nchi ikiwa hivyo inakuwa haiko salama na haitakuwa na amani na maadui wa chama wapo ndani ya chama chenyewe.

Pia alisema kiongozi aliyekomaa hawezi kuongelea kauli kama hizo upinzani si kitendo cha watu kununiana na kutosaidia kwa hali na mali.

Hata hivyo alisema kuwa alikwenda Mkoani Lindi kwa ajili ya kuupokea Mwenge na kwenda kuziba mashimo ambayo waliyochimba CHADEMA katika jimbo la Mtama.

Wakati huo huo,Waziri Membe alisema kuwa wameunda tume ya kuchungaza pesa zilizotolewa bila ya idhini ya Wizara hiyo.

Alisema kuwa tume hiyo imewahusisha wagakuzi wa mahesabu ya ndani, Takukuru, usalama wa Taifa pamoja na viongozi wengine kutoka wizarani.

 Hata hivyo Membe alisema kuwa pesa hizo zilitoweka Machi 1 ambazo zilikuwa bilioni 3.5 ambapo viongozi wote wa wizara walikuwa hawapo pesa hizo zilikuwa ni kwa ajili ya safari ya Rais Kikwete na viongozi wengine ambao waliokuwa wanaambatana na Rais katika safari hiyo.

Alisema kuwa mpaka hivi sasa pesa hizo tayari zimeshaonekana zipo katika akaunti ya Wizara hivyo ajahusishwa mti yeyote kuwa ameiba pesa hizo hivyo wataendelea kufanya uchunguzi ili wajiridhishe na kamati ikimaliza kazi yake watatoa taarifa kwa vyombo vya habari ili umma ujue hilo.

Pia alizungumzia mpango wa utawala wa kujitathimini (APRM)
ambapo alisema kuwa Rais atawasilisha ripoti Januari 2013 Nchini Adis ababa.

Alisema kuwa Tanzania haitajadiliwa Julai mwaka huu kama ilivyotakiwa kutokana na kwamba bado wageni waliokuja mwaka huu kufanya tathimini hawajaipitia ripoti ya Tanzania .

Alisema kuwa baada ya ripoti hiyo kupitiwa na umoja wa wa wananchama wa APRM watatuma maswali ili Tanzania waweze kuwajibu.



  

No comments:

Post a Comment