Wednesday, June 20, 2012

MBATIA AIRUSHIA KOMBORA TAASISI YA AGHA KHAN



Mbunge wa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, James Mbatia ameitupia kombora Taasisi ya Agha Khan kutokana na kupewa misahama ya kodi tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961.Mbatia alitoa kauli hiyo jana bunge alipokua akichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya 2012/13,ambapo alisema ili taifa liendelee ni lazima liangalie misamaha ya holela ya kodi zinazotolewa kwa taasisi binafsi


“Mheshimiwa Naibu Spika bajeti ya serikali si rafiki wa maendeleo ya Watanzania , kubwa ni kuwepo kwa misamaha ya kodi kwa mujibu wa taarifa zinaonyesha Taasisi ya Agha Khan, imekuwa ikisamehewa kodi tangu nchi hii ilipopata uhuru, lakini tunalalamika kukosa mapato ya serikali”

“Na hata kama tukiacha hili bado bajeti haitoijibu kwa hasa sekta ya miundo mbinu ya reli na barabara ambayo imetengewa kiasi kidogo cha fedha , ni kiasi kidogo cha fedha kimetengwa katika sekta ya barabara na kubwa kama serikali ingekuwa na nia njema basi hili wangelimaliza kwa makini kwa kukosa umakini huu leo hii foleni ya jiji la Dar es Salaam kila siku serikali inapoteza Sh. Bilioni 4”

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alisema bajeti ya serikali imejaa nadharia kuliko vitendo “Nashangazwa na michango inayotolewa na wabunge wa CCM eti na kudai bajeti ya kambi ya upinzani haina kitu na hili ni ushahidi toaha kwa chama kilichopo madarakani kupoteza dira na mvuto mbele ya watanzania

No comments:

Post a Comment