Monday, July 23, 2012

TAMARA: HATUJAWAI FANYA NGONO KWA ZAIDI YA MWAKA



 
Tamara ni Binti wa tajiri maarufu wa magari yanayojulikana kama F1 (Bernie)

Tamara afungua moyo na kunena kuhusu kuvunjika kwa penzi lake yeye na Omary Khyami
Tamara - ambaye ni mtoto wa bosi wa magari ( Formula One) kwa jina  Bernie Ecclestone - alisema kwa sasa anapata utambuzi kuwa kitendo cha Rafiki wake wa kiume  Omary Khyani kukataa kufanya tendo la ndoa kwa mda wote huo, limesababishwa na udanganyifu aliokuwa anaufanya na wanawake wengine nje.

Tamara mwenye umri wa miaka 28,alimtimua omary,38, kutoka kwenye jumba la kifahari walilokuwa wanaishi (mali ya Tamara) baada ya kuona mkanda wa video, alio pewa na baba, unaonesha vitendo vya aibu alivyokuwa anavifanya na wanawake wengine wakati wakiwa marafiki.

Tamara, ambaye atarithi £ 2.7billion alisema "wakati Omary akionesha kutokuwa na hamu ya kufanya ngono na mimi, niliuzunika sana na nikajaribu kufikiri kuwa nifanye nini?, pengine niendelee na utaratibu wa chakula (diet) au niende kwenye mazoezi ili nipunguze uzito.kweli alinifanya nijisikie kuwa mwnamke ambaye sijakamilika(not good enough) kwa mwanaume kama yeye.


Omar aliiambia gazeti linalojihusisha na mabo ya urembo kuwa, ilikuwa ni msongo wa mawazo alio nao uliomfanya asiweze fanya mapenzi na Tamara.

Mwanamitindo huyo Tamara alisema: "Kila kitu kingine katika uhusiano wetu kilikuwa kinaenda vizuri. Tulikuwa marafiki wazuri na mimi nilihisi kwamba yanayotokea kwa sasa katika uhusiano yetu, pengine ni hatua tu za kimapenzi kuwa yanapaswa yatokee na pengine yataisha baada ya mda kidogo.
“Lakini nikiangalia nyuma, najiona kuwa nilikuwa mjinga kwa mawazo hayo kwa sababu ilikuwa ni miaka miwili tu na nusu toka tuwe wapenzi na sio miaka 20.”

"Kuna haja ya kuwapo cheche za mapenzi kati yetu. Yeye Omary alikuwa ananiambia kuwa, anakuwa na kazi nyingi siku nzima na zinampelekea kutopata hamu ya kufanya mapenzi."

Omar mara ya kwanza baada ya mkando huo wa aibu kuonekana , alijaribu kujitetea kwa kusema  kuwa video hiyo walimchukua akiwa amelewa na ilikuwa kabla ya kuanza mahusiano yao.

Lakini Tamara alisema video hiyo inayomwonesha Omary akifanya vitendo vya ngono na wanawake wengine, ilionesha akiwa amevaa bangili ya dhahabu yenye thamani ya £ 30,000  mkononi, ambayo Tamara alimpatia Omary kama ishara ya Pendo la dhati kwake. 

Akiongea huku akitokwa na machozi, alisema: "Kulikuwa na dhahabu ya njano na nyeupe ambayo nilimnunulia kama zawadi wakati wa uhusiano wetu”.na hizo zote alionekana amezivaa wakati akiwa na wanawake hao kwa nyakati tofauti.


"Hivyo nilijua kuwa video hiyo ilikuwa  imechukuliwa wakati tukiwa pamoja kwenye mahusiano na si kama vile anavyodai kuwa ilikuwa kabla ya kuanza kwa uhusiano wetu. na kuwa katika wakati huo tumekuwa tukiishi pamoja, kulala katika kitanda kimoja kila usiku.

Baba yake Tamara, Bernie, alimpigia simu mwaneye na kumuita ofisini kwake mjini london baada ya kupatiwa mkanda na vyanzo vyake vya habari. Mama yake Slavica, 54, alikuwa pia hapo ofisini.

Tamara hakuweza kuamini kile alichokuwa anakiona  wakati mkanda huo ulipo anzwa kuoneshwa mbele ya baba yake mzazi.

Tamara alisema: "Nimejisikia kichefuchefu, mgonjwa. Ilinivuruga akili kwa kile nilichokuwa nakiona. Omar amenifedhehesha kuliko mtu yeyote ambaye nimeshawahi kukutana nae katika maisha yangu.

"Nilipata na mshtuko, na kukata tamaa. Sikuweza hata kufikiri kitu kama hichi kufanywa na Omar.Amenifanya nijisike vibaya kiasi cha kuumwa pindi napo mwona."

Wakati akiona video hiyo, Tamara alimpigia dada yake Petra, 22, na kumtaka aje ofisini kwa baba yake kuona jinsi Omar alivyomasliti kwa kufanya ngono na mwanamke mwingine. Lakini Petra alicheka, akidhani ni utani tu, lakini alipofika ofisini na kuona nyuso zenye uzuni alitambua kuwa alicho ambiwa na dada yake Tamara ni cha kweli.

Tamara alimpigia simu Omar kumuuliza yahusuyo na video aliyo iona.Omary kwanza alikana na baadae tena kidogo akakiri kuwa na kusema kuwa alikuwa kama ametekwa.Tamara akamwambia lakini hapakuwepo mtu aliyekuwa amekushikia bunduki kichwani kwako!!
Tamara alimwambia Omary. “Video aliyoiona ni ushahidi tosha wa usaliti wake kwake katika penzi”

baada ya hapo Tamara na dada yake Petra waliongozana kwenda nyumbani kwa tamara, kumsaidia kukusanya nguo na vitu vyake vyote vya Omary na kuvipeleka nyumbani alikokuwa anakaa kabla ya kukutana na Tamara.

Tamara alisema.” Siwezi kamwe kurudisha moyo wangu nyuma. Kuna mambo mengi naweza kusamehe na pia najua watu hufanya makosa ila kwa hili siwezi. Na najuta kumfahamu Omar.

sasa pia akili inanijia na kujuliza. Alipokuwa anasema yupo mazoezini, kwenye mikutano je ni kweli alikuwa huko?


" Namshukuru Mungu kwamba sijazaa naye na hatujafunga ndoa.

Tamara aliongeza: "Singependa Omar amuumize msichana mwingine kama alivyofanya kwangu. Kwani inaumiza sana na ni usaliti mkubwa sana."

mwisho kabisa Tamara katika mahojiano hayo, aliomba pesa zitakazopatikana katika kipindi hicho zipelekwe kusaidia Hospitali ya watoto wa mitaania ya mjini London (
London’s Great Ormond Street children’s hospital).

No comments:

Post a Comment