Monday, July 23, 2012
MUZIKI WA TANZANIA UPO KATIKA HADHI YA KIMATAIFA?
Baadhi ya wasanii wengi nchini Tanzania wanatamani kufanya muziki na kuipeleka fani hiyo katika ngazi ya kimataifa ingawa hawaonyeshi juhudi zozote katika kufanikisha hilo Ukifanya mahojiano na baadhi ya wasanii nchini Tanzania kila msanii ana ndoto na malengo ya kuupeleka muziki wake katika ngazi ya kimataifa huku wakiwa na kila sababu ya kuutangaza muziki wake katika mipaka ya ndani na njee ya nchi yetu huku akipeperusha bendela ya nchi hii
Lakini je wasanii hao hususani wanamuziki wa kizazi kipya wamefanya jitihada gani za kusababisha muziki wao kufika katika ngazi za kimataifa kama kutimiza ndoto zao na malengo yao waliyoyakusudia
John Kitime muimbaji wa The Kilimanjaro band yeye anasema kwamba Kosa kubwa wanalolifanya wasanii wetu hapa nchini ni kujivunia na mashahiri wanaamini kwa kutumia mashahiri wanaweza kufika katika ngazi ya kimataifa huku wakisahau na kupoteza dhana ya ubunifu
Anasema kuwa mashahiri peke yake hayatoshi kuupeleka muziki au sanaa yetu katika soko la muziki la kimataifa pamoja na kuvusha sanaa yetu katika ngazi ya kimataifa na kuufanya ujulikane dunia kote, ingawa wapo baadhi ya wasanii wanaopata shoo za njee ya nchi lakini kulingana na kujivunia au kutumia mashahiri wanajikuta wanafanya shoo zao hizo katika hadhira ya watanzania pekee
“Baadhi yao wanapata mialiko ya kufanya shoo nje ya nchi lakini wanaishia kuipigia hadhira ya watanzania wenzao na hapo ndipo utagundua muziki wetu upo katika ngazi gani , wasanii kama wakongo wanapokuja kupiga muziki kwetu wanapiga katika hadhira ya watanzanii na si ya wakongo kwa kuonyesha kwamaba muziki wao upo katika ngazi ya tofauti”
Wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu, kwani ubunifu ni kitu kipya ambacho mwanamuziki mwingine hana ila wewe unacho, hivyo ubunifu ndio ngazi peke ambayo msanii anaweza kutumia kwa kujinyanyua kufika katika ngazi anayoitaka ikiwemo kimataifa
Aliongezea kuwa baadhi ya wasanii hapa nchini wanapenda kuiga vyote vya njee na kusahau vya kwao hii husababisha kupoteza radha na vionjo vya muziki na ndio maana mpaka sasa bado hatuna muziki unaoweza kutambulisha nchi yetu
Kitime alisema kuwa hao tunaowaiga wasanii wenzetu wa njee wanalinda na kuuthamini utamaduni wao kwa kuchukua uwasili wao kwa kutumia katika muziki wao na ndio maana utakuta kuna nyimbo zinazotambulisha nchi kama Nigeria,
“Kwetu sisi ni tofauti kwa kujidai tumechanganyikiwa kwa kuchukua na kutumia midundo ya nyimbo za wenzetu wakati tulikuwa na uwezo wa kuchukua midundo ya ngoma za makabila yetu ya asili kama mdundiko na kujikuta tunapata kitu bora amabacho hata hao wa nje wanaweza kuiga kutoka kwetu”
Kitime anaongezea kuwa tatizo linalowakabili wasanii wengi nchini ni kutojitambua na kutojua thamani zao hii inasababisha wasambazi wa kazi zao kuwanyonya wasanii hao na kuendesha mfumo mzima wa soko la muziki hivyo husababisha msanii kushindwa kufika katika ngazi ya kimataifa kwani huyo msambazaji anaangalia soko linataka nini na si soko la ngazi ya kimataifa linataka nini
Alisisitiza kuwa ili muziki uingie katika ngazi ya kimataifa tunatakiwa tubadilishe mfumo mzima kwani wasanii wanataka kutoka ,wasambazaji wanataka faida bila ya kuanagalia uwezo wa msanii kwa hiyo wanachokifanya ni kuangalia ni aina ya nyimbo inayouza na si aina gani ya nyimbo ambayo inaweza kukupeleka kimataifa
Labels:
Burudani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment