Wednesday, June 20, 2012

BOBBY BROWN AMEOA KWA MARA NYINGINE TENA.

Bobby Brown na  mke wake mpya Alicia Etheredge wakiwa katika picha ya pamoja baada ya harusi yao iliyofanyika  mji wa Hawaii Jumatatu.


Mume wa zamani wa mwanadada Whitney Houston, Mwenye umri wa miaka 43, amemuoa meneja wake, Alicia Etheredge, katika harusi iliyofanyika mjini Hawaii Jumatatu, iliripotiwa.
 
Chanzo hicho kimeelezea kwmaba Bob Brown waliingia kwenye uchumba mwaka 2012 wakati wa mauzo ya  New Edition katika Jacksonville, Fla.

Mtoto wa kiume wa Brown mwenye umri wa miaka 19, aitwae Bobby Jr,ameweka picha za harusi hiyo kwenye mtandao wa kijamii ujulikanao kama  Twitter.

Picha hiyo pia inaonyesha Brown amevaa suti nyekundu na Adidas sneakers, wakati Etheredge amevaa vazi la harusi lijulikanalo kama shela ya harusi.

Familia nyingine ambaye pia alijiunga katika siku ya maadhimisho ya Brown walikuwa watoto wakubwa, Landon, 23, na La'Prinicia, 22.

Hata hivyo, Bobbi Kristina Brown Binti ya Houston  hakuwepo wakati wa harusi. 

No comments:

Post a Comment