Sunday, July 22, 2012

MAREKANI YAPUNGUZA MISAADA YA KIJESHI KWA SERIKALI YA RWANDA



Marekani imepunguza misaada ya kijeshi kwa Rwanda kufuatia  madai yake kuwa inaunga mkono waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Idara inayohusika na maswala ya fedha kutoka Ikulu ya Marekani imesema kiasi cha fedha  
 $ 200,000  sawa million  316,100,000 za kitanzania zilizokuwa zilizokuwa zikipelekwa katika Serikali ya Rwanda zitagawiwa kwenye nchi nyingine.

Rwanda ilikanusha kuunga mkono kundi lijulikanalo kama M23 kwenye taarifa iliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa.
Watu zaidi ya  200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo yanayoendelea huko mashariki ya DRC Kongo.

Historia fupi ya mapigano katika ukanda huo:

 
Aprili-Juni 1994: Mauaji ya Kimbari ya Watutsi nchini Rwanda
Juni 1994: Watutsi wakiongozwa na Paul Kagame wachukua madaraka Rwanda, wapiganaji wa Kihutu   wakimbilia Zaire (DRC)
Jeshi la Rwanda inaingia mashariki mwa Zaire kupigana na  waasi wa Kihutu waliokimbilia Zaire
 
1997: Laurent Kabila(AFDL), akiungwa mkono na jeshi la Rwanda atwaa madaraka mnjini Kinshasa 
1998: Rwanda inamtuhumu Kabila kwa kutowakabili waasi wa Kihutu, Majaribio ya kutaka kumpindua yanafanyika na hivyo kuzua  miaka mitano ya vita nchini DR Kongo.
2003: mwisho wa vita ndani ya DR Kongo, lakini bado Wahutu na wanamgambo wa Kitutsi waliendelea na mapigano  mashariki mwa DR Kongo.
2008: Kitutsi inasaidia waasi wa CNDP kuelekea mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma - watu 250,000 kukimbia 
2009: Rwanda na Kongo DR waingia makubaliano ya amani,waasi wa  CNDP  kuingizwa katika jeshi la Kongo 
2012: Uasi waibuliwa upya  nchini kongo na  kiongozi wa CNDP Bosco "Terminator" Ntaganda

Ukanda wa Mashariki mwa Kongo DR umejiingiza katika mapigano tangu mwaka 1994, wakati zaidi ya Wahutu millioni moja wenye msimamo wa kikabila walivuka mpaka na kuingia DR Kongo kufuatia mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ambapo baadhi ya watu 800,000 - wengi wao wakiwa Watutsi - walikufa.

Rwanda mara mbili walivamia DRC Kongo, kwa madai kuwa alikuwa anajaribu kuchukua hatua dhidi ya waasi wa Kihutu katika DR Kongo. Uganda pia ilishawahi kupeleka  askari katika DR Kongo wakati wa vita 1997-2003.

Repoti ya hivi kribuni iliyosomwa na televisheni ya BBC , imeseonesha kuwa serikali ya Rwanda inasaidia waasi wa M23.

Ripoti ilimnukuu askari wa Rwanda ambaye alijiondoa  kutoka majeshi ya waasi wa Kongo.askari huyo aliiambia UN kuwa walikuwa wakipatiwa mafunzo nchini Rwanda kama gelesha ya kujiunga na jeshi la Rwanda , lakini baadae walikuwa wanapelekwa mapakani kujiunga na waasi wa M23.

Serikali ya Rwanda alikanusha madai hayo.

Waasi wa Kongo hao wajulikanao kama M23, wamejiingiza katika uasi baada ya kushindwa kuendelea na makubaliano ya amani yaliyotiwa  saini na serikali ya DR Kongo tarehe 23 Machi miaka mitatu iliyopita.

Wengi wa waasi hao ni wakabila la Kitutsi – kama ilivyo katika uongozi wa Rwanda.

No comments:

Post a Comment