Kutotolewa kwa elimu ya UKIMWI katika vituo vya afya na wafanyakazi wake ni hali inayochangia kuenea kwa ugojwa huu kwa kasi kwani wao ndio wasambazaji wakubwa katika jamii.
Jamii inatakiwa kuelewa juu ya elimu ya UKIMWI na elimu hiyo wanatakiwa kuipata katika vituo vya afya pale wanapokwenda kufuata huduma zao mbalimbali.
Lakini ni hali ya kushangaza mpaka leo hii wapo wafanyakazi wanaofanya kazi katika vituo vya afya hawana elimu ya UKIMWI kama vile inavyotakiwa .
Jamii inatakiwa kupata elimu ya ufahamu juu ya ugojwa wa UKIMWI ili waweze kuepukana nao na hata kuwahudumia wale ambao walioathirika na ugojwa huo.
Jamii kubwa imekuwa na unyanyapaa kutokana na kukosa elimu ya UKIMWI,kwani mpaka leo hii zipo baadhi ya familia humtenga mtu aliyeathirika na ugojwa huo na kutoshirikiana naye katika kitu chochote kile ambacho kinacholeta maendeleo.
Unyapaa huo huanzia kwanza kabisa katika vituo vya afya na kumalizikia katika jamii tunazoishi bado watu hawajaelimika kuhusu suala zima la UKIMWI.
Ukiangalia hata katika vituo vyetu vya afya jinsi vilivyojengwa ni hali inayoonyesha kuwa unyanyapaa umegusa, kwani hakuna kituo cha afya kilichojenga jengo la kutolea huduma ya UKIMWI karibu vituo vyote vya kutolea huduma hiyo vimejificha nyuma ya kituo cha afya.
Hali hiyo inaonyesha hata katika ujenzi wa vituo hivyo elimu haikutumika kwani ugojwa wa UKIMWI ni sawa na ugojw amwingine haikustahili majengo hayo kujengwa nyuma ya majengo mengine.
Pia hali hiyo inasababisha hata wagojwa ambao wanaohitaji kwenda kupata huduma katika vituo hivyo kushindwa kwenda kwa kuwa ukionekana unakwenda maeneo hayo kila mmoja anaanza kukunyooshea kidole.
Watu wengi hukwepa kwenda kutibiwa karibu na kituo kilicho karibu naye na hufunga safari kwenda kutibiwa sehemu nyingi ili asionekane na watu kuwa anakwenda kufuata huduma hiyo.
Wagojwa wengi ambao wanaohitaji huduma ya UKIMWI mara nyingi hutibiwa sehemu ambayo haishi kwa kuogopa unyanyapaa kwa watu wanaowafahamu na hata wale wanaotoa huduma ambao anatia shaka anaweza kuwa anamjua.
Yupo mgojwa ambaye anaishi Mkoa wa Morogoro lakini matibabu yake hupata Dar es Salaam kwa kuhofia hunyanyapaa ile sehemu anayoishi.
Anasema kuwa anaogopa kupata huduma sehemu anayoishi kwani anaogopa unyanyapaa na kunyooshewa vidole na watu .
"Mimi ni mfanyabiashara wa vyakula sasa watu wakiniona kuwa tayari nimeathirika hata biashara yangu hawatanunua na vilevile nitakuwa natengwa katika shughuli za kijamii, kwani wapo ambao wanaojulikana lakini jamii huwatenga kwa kila kitu ndio maana nimeamua kuja kuchukua huduma huku mbali ili nisijulikane na mtu"alisema (hakutaka kutaja jina lake)
Hali nayo inaongeza idadi ya wagojwa katika hiyo sehemu kwani utakuta sehemu hiyo inawakazi wachache lakini watu ambao wanaopata huduma hiyo ni wengi kuliko wakazi wanaoishi hapo.
Pia hilo nalo linasababisha wagojwa kukosa huduma ya dawa kwa wakati mwingine dawa zinazochukuliwa ni chache tofauti na wagojwa wanaokwenda kupata huduma katika kituo hicho.
Tukija kwa watoa huduma wa afya nao wengi wao elimu ni ndogo kwani hata makaribisho yao pale mtu anapotaka kwenda kupima afya moja kwa moja unajua kuwa mtu huyu ajapata elimu ya UKIMWI.
Vile vile vipo vituo vya afya ambavyo vinampima mtu bila hata ya kumpa ushauri na nasaha, unaotakiwa kwa mtu anayekwenda kupima afya yake.
Hata ukienda hospitali kama unasumbuliwa na tumbo au kichwa lakini ni lazima mtoa huduma wa kituo hicho atakuuliza kama tayari umeshapima UKIMWI.
Ukimjibu kuwa bado ujapima anakwambia ni lazima ukapime kwanza halafu huduma zingine ni baadaye, kwani hilo inabidi elimu ya UKIMWI itolewe kwa wingi na kwa namna mbalimbali ilimradi kila mtu apate elimu hiyo ya uafahamu.
Kwa hivyo hapo kunakuwa hakuna elimu yeyote ya ushauri nasaha inayotolewa kwa mtu anayehitajika kupima afya yake.
Hali hiyo ndio inayosababisha mtu kutopokea majibu yake na hata akipokokea huchanganyikiwa na wakati mwingine huweza kufariki dunia gafla kwa sababu ya mshutuko.
Inatakiwa kama mtu amefika katika kituo cha afya apewe ushauri kwanza baada ya hapo ndipo aweze kupimwa kwa kuwa anakuwa ameshatayarishwa hata akipokea majibu yeyote yale anakuwa hana wasiwasi wowote wa kupokea majibu yake vile itakavyokuwa.
No comments:
Post a Comment