Wednesday, June 20, 2012

RAY HAJUI URAFIKI WA MAREHEMU KANUMBA NA LULU

Msanii wa filamu nchini maarufu Vincent Kigosi 'Ray' amesema kuwa kifo cha msanii marehemu Kanumba akikusababishwa na yeye kwani siku mbili kabla ya kifo chake wazazi wa marehemu waliwasuruhisha na kumaliza tofauti zao


Hayo yalisemwa Dar es Salaam na msanii wa filamu katika mahojiano ya kipindi cha mikasi, Ray alisema kwa kuwa wazazi wa marehemu walituweka pamoja na kutusuruhisha kwa kile kilichotokea kati yetu na kuweka mambo sawa mimi nilikuwa sina mengine

"Ilikuwa siku ya Alhamisi tulisuruhishwa nyumbani kwa marehemu ili tuendeleze upendo kama ulivyokuwa  na baada ya siku mbili mwenzangu akafariki dunia ghafla " alisema Ray

Aliongezea kuwa urafiki wao ni wa muda mrefu toka wanaishi Tandika jiojini Dar es Salaam wakati huo kwa pamoja tulikuwa tunatafuta maisha

Hata hivyo msanii huyo alisema hafahamu chochote kuhusu urafiki wa msanii Lulu na marehemu Kanumba wala hajui chochote kilichotokea kati yao

Pia alisema mpaka hivi sasa hana mke wala hana mtoto wa kusingiziwa na hajakutana na mwanamke miezi saba iliyopita


No comments:

Post a Comment