Baada ya kushindwa kupatikana kwa muafaka kati ya Serikali na madaktari hivyo madaktari wameamua kutangaza mgomo usiokuwa na kikomo kuanzia kesho. Mgomo huo ambao utakaohusisha madaktari wa ngazi zote, kwa kuwa serikali haijatimiza kile walichokuwa wanakiitaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Dkt. Stevev Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania alisema kuwa Serikali ya Tanzania inapenda zaidi migogoro kuliko suluhisho.
"Leo ndio mwisho wetu wa kutoa huduma kwani tunaona wazi kuwa serikali haitujali ndio maana hawataki kututekelezea madai yetu tunayodai"alisema Dkt Ulimboka.
Aliongeza kuwa Waziri Mkuu anathubutu kusimama bungeni na kusema maneno ya uongo ili sisi jamii ituelewe vibaya hakuna dai lolote tulilolipendekeza na waliotutekelezea.
Hivyo alisema kuwa hawataogopa kwenda sehemu yeyote kushitaki sisi msimamo wetu ni huo huo.
Alisema kuwa Waziri mkuu amekazania posho ya uchunguzi wa maiti kuwa wameiongeza kutoka sh..10,000 mpaka 100000 dai hilo hapo mwanzo tulikuwa hatujaliandika lakini walivyotuletea majibu tulishngaa limewekwa.
"Wameweka dai hilo kwa makusudi kwani hapa Tanzania madaktari hata kumi hawafiki ambao wao ndio hufanya uchunguzi wa maiti na inakuwa si mara kwa mara,daktari unaweza kuanza kazi na mpaka ukastaafu hata mara moja uiifanyie uchunguzi maiti."alisema Ulimboka.
Naye, Katibu wa Jumuiya ya madaktari Dk Edwin Chitage alisema kuwa,, Serikali inatudharau labda kwa sababu ilikaa na sisi kitu kimoja kwa ajili ya majadiliani sasa ni bora kuludi tulipotoka.
Alisema kuwa Tuliagana vizuri na waziri mkuu lakini tunashangaa majibu waliyojibu yanashangaza na inaonekana kuwa wanatudharau..
" Tumeshangazwa na majibu waliyotoa kwani hakuna hata jibu moja ambalo lililohusiana na huduma za afya ambako ambako mpaka hivi sasa hospitali ya Taifa Muhimbili aina kipimo cha T-SCAN hata wagojwa wanaopewa rufaa kuja hospitalini hapo kwa ajili ya kufata kipimo hicho na wakifika hapo hupewa rufaa waende katika hospitali za binafsi ili kwenda kupima kipimo hicho."alisema Dkt Chitage.
Aliongeza kuwa kwa sasa ni miezi saba kipimo tangu kiharibike lakini hakuna suluhisho lolote linalotolewa dhidi ya kuwatesa watanzania hasa wale wenye uwezo mdogo..
Hata hivyo Makamu Mwenyeti wa jumuiya hiyo Dkt.Godbles Charles alisema kuwa,katika kipindi hicho cha mgomo watakaa pamoja ili wawe wanatibia wagojwa wa dharura kama vile wajawazito, na wale wanaotakiwa kufanyiwa operesheni.
Naye, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliiambia bunge kuwa tayari madai matano ya madaktari wameshayatimiza.
Bw. Pinda alisema kuwa kama mgomo hutafanyika mgomo huo hautakuwa wa kisheria kwani mpaka hivi sasa tunasubiri chombo cha majadiliano (CMA) tujue watasema nini juu ya hilo.
No comments:
Post a Comment