WAFANYAKAZI wa wizara ya fedha wametakiwa kushirikiana katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kuongeza uwezo wa serikali katika kutoa huduma bora zaidi kwa wanachi . Hayo yalisemwa na waziri wa fedha Bw. William Mgimwa wakati akifungua mkutano maalum wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo Dar es Salaam jana Alisema changamoto hizo ni pamoja na kuwepo na mfumuko wa bei ambapo umepanda mpaka kufikia 2 digts ,ambayo imesababishwa na upandaji wa vyakula ikiwemo mchele, sukari na unga kwani hivyo ndivyo vinavyotumiwa na wananchi wote
Alisema ili kuhakikisha mfumuko wa bei unashuka na kudhibitiwa lazima waboreshe miundo mbinu hasa barabara ili kuhakikisha chakula kinafika kwa wakati na pia kuruhusu sukari ingizwe kwa wingi sokoni.
Kwa upande mwingine aligusia suala la urekurekebishaji wa sheria ili kuongeza mapato ya nchi ili kuepuka uwekezaji ambao unaleta hasara hivyo wizara inaweka mikakati ya namana gani ya kuiboresha ili waweze kufanikiwa.
“Tumegundua kuna maeneo ya uwekezaji hayandi vizuri kwa kuwa wahusika wanabadilishana rasilimali walizowekeza hapa nchini bila serikali kufaidika hivyo sheria hii itaangalia jinsi mabadilishano yanavyokuwa ili kuhakikisha serikali inapata mapato maeneo ya uwekezaji ”alisema
Aliongezea kuwa , mpango wa mda mrefu wa kuboresha uzalishaji ni lazima tuwe na umeme wa uhakika kwani uwekezaji wote wa mjini na vijijini unaendeshwa kwa nguvu za umeme
“Tumeshapata muwekezaji tumempeleka mtwara na tushaingia naye mkataba wa dola milioni 60 fedha hizo ni sehemu ya miradi tunawekeza katika bomba la gesi” alisema
No comments:
Post a Comment