Friday, August 3, 2012

MATOKEO YA MICHEZO - AFRIKA MASHARIKI KATIKA OLIMPIKI

Matokeo ya awali ya michezo mbalimbali ambayo imefanyika leo Mjini London, inayohusisha wachezaji kutoka Afrika Mashariki.
hata hivyo kwa Upande wa Tanzania, hatukuwa na mshiriki hii leo.

Wakimbiaji kutoka kenya ndio waliofanya vizuri na wawili kati yao wataingia kwenye robo fainali za mashindano hayo




Nchini Kenya, Vincent Kiplangat Kosgei, Mwenye miaka 23 ameweza kushika nafasi ya 7 katika mbio za mita 400 kwa Wanaume.Mkimbiaji huyu amatumia sekunde 50:80



 
Boniface Mucheru mwenye miaka 20 kutoka Kenya ameshika nafasi ya 6 kwa mbio za mita 400 kwa wanaume, akitumia sekunde 50.33

Joy Nakhumicha Sakari mwenye umri wa miaka 26, ameshika nafasi ya 3 katika mbio za mita 400, akitumia sekunde 51.85.
 Mwana dada huyu kutoka Kenya kesho taraehe 4th August 2012 anaingia kenye robo fainali ya mashindano haya.


Abel Kiprop Mutai,Umri miaka 23, ameweza kukimbia kwenye mashindano ya mita 3000, nakushika nafasi ya 3 kwa upande wa wanaume, akitumia dakika 8:17:70
Tarehe 5th August 2012 anaingia kwenye robo finali za mbio hizi.

BURUNDI:
Elsie Uwamahoro, umri miaka 23, ameweza kushika nafasi ya nne katika mashindo ya kuogelea katika umbali wa mita 50,akitumia sekunde 33.14





Alphonsine Agahozo, kutoka Rwanda, umri miaka 16 leo ameshindana katika kuogelea umbali wa mita 50 na kushika nafasi ya 3 akitumia sekunde 30.72.

UGANDA:
Jamila Lunkuse , umri miaka 15 tokea Uganda, ameweza kushika nafasi ya 8 katika mashindano ya kuogelea umbali wa mita 50, akitumia sekunde 28.44


 Benjamin Kiplagat, kutoka Uganda, umri miaka 23, ameshika nafasi ya 6 katika mashindano ya mbio za mita 3000 kwa upande wa wanaume, akitumia dakika 8:18.44

Tarehe 5th August 2012 anatarajia kuingia kwenye robo fainali za mashindano hayo.


Jacob Araptany, kutoka Uganda, umri miaka 18, ameshika nafasi ya saba katika mbio za mita 3000 kwa upande wa wanaume, na kushika nafasi ya 7 akitumia dakika 8:35.85.



No comments:

Post a Comment