Hospitari ya Regency ya Dar es Salam imeanzisha program
kabambe ya upasuaji wa maradhi
mbalimbali ya tumbo kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kutumia kamera, ambapo
mgonjwa hapasuliwi sehemu kubwa.
Upasuaji huo unahusisha kupasua tundu dogo kwenye tumbo na
kuingiza kifaa chembambe tumboni, ambacho huonesha picha ya tatizo husika
kwenye televisheni na hatimaye daktari kufanya matibabu bila kupasua sehemu
kubwa ya tumbo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency, Dkt. Rajni
Kanabar, utaratibu huo mpya utapunguza gharama kwa wagonjwa kwenda India na
nchi mbalimbali kwa ajili ya upasuji wa aina hiyo, ambao ndio kwanza
umeanzishwa na hospitalini hapo.
“Badala ya kwenda nje ya nchi, kwa ajili ya upasuaji huu wa
kisasa watu watapata fursa ya kufanyiwa upasuaji hapa hapa nchini, hii itaokoa
fedha na muda na tangu tuanze huduma hii miezi miwili iliyopita wagonjwa 35
wameshapasuliwa na wanaendelea vizuri,” alisema Dkt. Kanabar.
Daktari bingwa anayefanya upasuaji huo, Dkt. Rajeev Tandon,
alisema kwa upasuaji wa kawaida daktari hutegemea kufanya upasuaji mkubwa ili
kufikia viungo anavyohitaji tumboni hali ambayo husababisha maumivu makali kwa
mgonjwa na kutopona haraka.
“Upasuaji huu wa kisasa tunaofanywa hapa Regency, unamfanya
daktari kufikia viungo anavyotaka kupitia matundu madogo tumboni, hii inasaidia
mgonjwa kubaki bila makovu baada ya kupona, kupona haraka na kuendelea na
shughuli zake saa moja tu baada ya upasuaji tofauti na upasuaji wa kizamani
ambapo humchukua muda mrefu mgonjwa kupona,” alisema, Dk Tandon
Mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa aina hiyo Juni
21, mwaka huu, alisema alikuwa akisumbuliwa maumivu makali na kutapika kwa
miezi kadhaa, lakini baada ya upasuaji anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment