BENKI ya NMB inatarjia kudhamini mashindano yatakayoendeshwa na Maisha Plus kwa kushirikiana na Oxfam kwa kuwashirikisha washindi walioshinda katika kampeni ya Mama shujaa wa chakula iliyoendeshwa na Oxfam .
Akiongea na wandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mark Wiessing alisema NMB imeamua kudhamini mashindano hayo ili kuhakikisha ardhi iliyopo inamsaidia Mtanzania mwenyewe kwani kupitia shindano hilo litawahamasisha watu kujishughulisha katika mambo ya kilimo
"Kwa kuakikisha NMB inawajali wakulima wadogo wadogo imeanzisha NMB foundation ambayo mbali na kutoa elimu pia inawahamasisha kujiwekea akiba na kukopa kupitia NMB
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Bw.Masoud Kipanya alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidogo na yaliyopita kwani idadi ya washiriki itaongezeka kutoka 18 miaka ya nyuma mpaka kufikia 26 mpaka 30 mwaka huu.
Alisema washiriki watakaa siku 14 na kuanzia wataanza na wanawake walioshinda katika kampeni ya mama shujaa wa chakula ambao watakaa siku 11 na siku tatu zitakazo baki watawajumuisha na washiriki wengine.
"tumeamua kushirikiana na mama shujaa wa chakula ili kumuenzi mwanamke ambaye ndiye mkulima mdogo ambaye mzalishaji mkuu wa chakula na kuwafanya vijana waweze kujifunza na kufikiria umuhimu wa uzalishaji wa chakula"alisema Bw Kipanya
Alisema usaili unatarjia kuanza jumatatu ijao kwa kupitia zile sehemu ambazo wametoka washindi wa mama shujaa wa chakula kwa kuonyesha dokumentari itakayoonyesha wakulima hao shughuli zao walizokuwa wananzifanya katika uzalishaji wa chakula.
Naye Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Bi Monica Gorman alisema lengo la kushirikiana na maisha plus ni kuweza kuwafanya wananchi wawaone wanawake hao kivipi wameweza kulima na kujipatia chakula chao cha nyumbani na biashara.
"wanawake hawa wamejitahidi sana kuondoa umasikini,njaa na hali ya kutokwa na kazi ya kufanya kwa kulima huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali .
No comments:
Post a Comment