Wednesday, August 22, 2012
PRECISION AIR YATOA MSAADA
KAMPUNI ya usafirishaji wa anga ya Precision Air imetoa msaada wa dola za kimarekani 3500, ambazo ni sawa na shilingi milioni 5.5 kwa fedha ya kitanzania kwa kituo cha watoto cha Don Bosco kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya mpira wa kikapu ya Afrika Mashariki
Msaada huo ambao utawezesha vikosi vya timu ya Mpira wa kikapu Savio na Don Bosco Lady Lions kuapata mahitaji na shughuri zote zamaandalizi ya michuano hiyo itakayoanza 20 mwezi huo nchini Kampala Uganda
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo Meneja wa Uhusiano wa Precision Air Bi. Annette Nkini alisema kuwa michezo inachukua sehemu kubwa katika jamii na kuwa sehemu mojawapo ya kuongeza kipato
“Tunayofuraha kuwa sehemu ya mafanikio ya timu hizi kwani wamefanya jitihada na tunawatumia kwenda kuwakilisha taifa na kutufanya tujivunie mafanikio yao” alisema
Aliongezea kwa kutoa wito katika kampuni nyingine kujitokeza kusaidia timu zinazofanya vizuri ili kukuza michezo katika nchi yetu
Kwa upande wa mkurugenzi wa kituo hicho Padri Frederick Swai alisema kuwa wamejianda vyema na kuhakikisha kuwa wanaipeperusha bendera ya nchi vyema katika mashindano hayo kwa kufanya vizuri
Alisema kuwa kwa kupitia msaada huo utawawezesha kufikia malengo yao kwa kujikwimu kimalazi kwa kila mchezaji pamoja na vitu vyote vya muhimu na kuweza kuikamilisha safari hiyo ambayo wanatarajia kusafiri kesho na timu mbili za jeshi
Alitoa wito kwa kampuni nyingine kuziangalia timu zinazofanya vizuri kwa kuzipa msaada ili kuweza kuziendeleza kimechezo
Timu ya Savio iliibuka mshindi wakati wa michuano ya kitaifa ya mwaka 2012 kwa wanaume huku Don Bosco Lady Lions waliibuka kama washindi wa pili kwa wanawake na kufuzu kushiriki michuano hiyo
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment