Friday, July 27, 2012
TRA YATOA ORODHA YA MAFUNDI KIELEKTRONIKI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa orodha ya mafundi ambao watashughulika kusimamia mashine za stakabadhi za kielektroniki(Electronic Fiscal Recepients) kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA ilieleza kuwa yatatolewa majina ya mafundi chini ya waajiri wao, ambao ndio watakao kuwa na kibali cha kuhudumia mashine za wateja wao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo majina hayo yatatangazwa kwenye vyombo vya habari kuanzia Agosti mosi, mwaka huu.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu, Bw.Allan Kiula, alitoa onyo kwa wateja ambao si waaminifu na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria.
Alisema kama kutakua na tatizo lolote kwa mteja basi awasiliane na fundi anayehusika. Aliongeza kuwa kuna wasambazaji wanaotakiwa kupewa taarifa hivyo hata zikiharibika ni lazima watumie muda mfupi kutatua tatizo.Aliwatahadharisha watumiaji wa mashine hizo kutojihusisha na mafundi tofauti na watakaotajwa na TRA.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment