Irone Dome- Kifaa amabacho Kwa mpango wa Israel kilipaswa kianze kutumika mwaka 2013, lakini kutokana na mashambulizi ya Hamas katika miji muhimi nchini Israel, imepasa kukizindua mapema hata kabla ya muda wake.
Kifaa hicho ambacho kipo kwa muundo wa kombora, kazi yake kubwa ni kuyapiga makombora na kuyalipua kabala hayajafika katika maeneo yalipoelekezwa na kuleta madhara.
Mapambano haya yameingia siku ya tano.
Israel imesema Kundi la Hamas linajificha kwenye maeneo ya raia, na hivyo kusababisha Israel isiwe na njia nyingine zaidi ya kuwafuata walikojificha.
Plan ya Israel kuingiza askari wa miguu ipo kwenye meza, ina subiri maamuzi.
Kundi la Hamas linasema halito simamisha mashambulizi yake mpaka hapo Israel itakapo kubali kutoendelea na ujenzi wa ukuta ukanda wa Gaza.
Israel nayo imesema makubaliano ya kusimamisha vita yasiwe na masharti yeyote.
No comments:
Post a Comment