Asasi ya Sober Tanzania imeandaa mkakati kabambe kusaidia
jitiada za Serikali zinazolenga kukomesha utumiaji na biashara za dawa ya
kulevya inchini.
Hatua hiyo imefikiwa wakati viongozi wa Serikali na vyombo
vinavyodhibiti utumiaji wa dawa za kulevya wakilalamika kukua kwa kasi kwa
biashara na utumia wa dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali nchini.
Akinguzindua sherehe za kuadhimisha Siku ya Kupinga Utumiaji
wa dawa ya kulevya duniani, hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu
alisema; “ Utumiaji na biashara ya dawa za kulevya ni tishio kwa nchi yetu,
tatizo hili linazidi kukua licha ya jitiada zinazofanywa kulipunguza.”
Akizungumza na waandishi jana, Katibu Mkuu wa Shirika la
Sober Tanzania, Bw. Fabian Nkingwa,
alisema shirika lake limeweka mpango mkakati wa kupambana na matumizi ya
biashara za dawa za kulevya.
Alisema mikakati hiyo inalenga kutomeza utumiaji wa dawa za
kulevya kwa ujumla wake, ikiwa ni pamoja na kukomesha utumiaji wa pombe za aina
zote miongoni mwa Watanzania.
“Si tumekwenda mbali zaidi badala ya kupambana na matumiza
ya dawa za kulevya peke yake, sisi tunajaribu kupinga matumizi ya pombe. Kwetu
sisi, pombe ni moja ya dawa ya kulevya, ambazo matumizi yake yanapaswa
kukomeshwa,” alisema.
Ili kufikia malengo yake, Katibu Mkuu wa Sober Tanzania,
alisema shirika limeandaa mikakati
mikali ya kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya dawa za kulevya, ikiwa ni
pamoja na pombe.
Kama sehemu ya kampeni hizo, Bw. Nkingwa alisema Shirika la
Sober Tanzania linahamasisha vijana kuunda vikundi kama vile klubu na kuelimisha jamii kuhusua madhara
yanayotokana na utumiaji wa dawa ya kulevya na mbinu za kujinasua katika
utumiaji wa dawa hizo.
No comments:
Post a Comment