Zaidi ya watu 28 waliokuwa wakisafiri na meli ya Mv Scarget kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar wamekufa na wengine 130 kuokolewa baada ya meli hiyo kuzama kusini mwa kisiwa cha Chumbe, visiwani Zanzibar
Taalifa ambazo amezipata mwandishi wa blog hii ni kwamba hadi jana saa 12 jioni zilisema idadi ya waliokufa katika ajali hiyo inatarajia kuongezeka kutokana na meli hiyo kuzama kabisa kwenye maji hivyo kutoonekana katika uso wa bahari,Maiti zilizofikishwa nchi kavu jana jioni ni pamoja na watoto watatu wa kiume na wanawake wanne akiwemo mzungu mmoja
Taarifa za kuzama kwa meli hii zilithibitishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Dkt. Mwinyihaji Makame wakati akizungumza na waandishi wa habari watu waliookolewa walifikishwa katika bandari ya Zanzibar
Kauli ya Waziri wa mambo ya ndani Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea na TBC1 alisema kuwa “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi alisema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”
No comments:
Post a Comment