Wanasayansi wametangaza matokeo ya awali kuwa mseto
mpya wa dawa tatu umeonyesha ufanisi katika kutibu ugonjwa wa kifua
kikuu, ugonjwa ambao unaua watu milioni moja na nusu kwa mwaka duniani,
ukiongoza kwa kusababisha vifo pamoja na Ukimwi.
Matokeo ya majaribio ya kwanza yameonyesha kuwa
mchanganyiko wa dawa hiyo unafanyakazi kwa ufanisi zaidi ikilinganishwa
na dawa zinazotumika sasa.
Watafiti wanasema majaribio ya wiki mbili
yaliyofanyika Afrika Kusini yameonyesha kuwa mchanganyiko wa dawa hiyo
mpya ilionyesha ufanisi kwa asilimia 99 katika kuua vijidudu vya TB.
Ufuatiliaji wa dawa hiyo kwa kipindi kirefu umeanza.
source:bbc swahili
No comments:
Post a Comment