Mamlaka ya Nchi kavu na Majini (SUMATRA) imetoa onyo kali kwa wamiliki wa daladala na madereva wao kwa kuwanyang'anya leseni na magari kutotembea kabisa barabarani pale watakapobainika kuwa magari yao yanamakosa ya kujirudiarudia.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shao, alisema kuwa wameamua kuchukua hatua kali hiyo ni baada ya madereva wa daladala kurudiana makosa hayo kila siku.
Alisema kuwa madereva wa daladala wamekuwa wakiwapa usumbufu abiria hasa wakati wa jioni kwa kupandisha nauli na kukatisha ruti hasa Barabara ya Bagamoyo,Barabara ya Nyerere,Barabara ya Ally Hassan Mwinyi,Barabara Morogoro,madaladala yanayopita njia hizo mara nyingi yamekuwa hayafiki kule yanapoenda mara nyingi huishia njiani na kusumbua abiria.
"Wamiliki wa daladala wanatakiwa kuwasimamia madereva wao na kuwapa onyo kila wakati na sikutegea SUMATRA au jeshi la polisi na kama dereva hawezi kufatiza masharti anayopewa na SUMATRA ni bora aache kazi ya udereva"alisema Bw.Shao.
Hata hivyo Bw. Shao alisema anashirikiana vizuri na abiria kwa kuwapa taarifa kwa madaladala yanayokatisha ruti na kupandisha bei ya nauli hasa wakati wa jioni.
Pia alisema magari yanayokatisha ruti na kupandisha nauli kiolela ni yale yasiyokuwa na leseni hivyo tukonayo sambasamba ili kuhakikisha yasitembee kabisa barabarani.
Aliongeza kuwa jumla ya magari 101 wameyakamata katika operesheni yao iliyoanza Julai 18.
No comments:
Post a Comment