Tuesday, July 24, 2012

JE!!?? RAISI KASAINI SHERIA MPYA YA MAFAO NSSF???!!!

Kuna habari zinaendelea kuzungumzwa kuhusu sheria mpya ya mafao ya NSSF kuwa, kwa sasa ili uweze chukua pesa yako inabidi uwe umetimiza miaka 55, hiyo ni kwa hiari na kwa lazima ni miaka 60.

na hiyo act inasema" ''This act shall apply to a person or employee employed in the formal or informal or self-employed in the mainland Tanzania and shall not apply to a person who has been insured or registered under any other law.''

habari hizi zinaendelea kusema kuwa , sheria hii haitawagusa wabunge au viongozi wa juu serikalini???

Uvumi huu unasema kuwa, Ukifa familia itaruhusiwa kuomba pesa zako, au ukiumwa ile mpaka wakaona unataka kufa..ndo wata kupa pesa yako..mmmh..
kuna maswali ya kujiuliza

Kwanza life span ya Mtanzania wa kawaida ni miaka mingani ?
watu kufika 55 wengi wetu tumechoka kabisa.

Pesa hiyo itakuwa na thamani kwa wakati huo?

kwa nini wafanye maamuzi bila kutushirikisha wadau?

tunaomba maoni ya watu kuhusu hili swala kama lipo..na limefikia wapi?

jambo hili limezungumziwa pia kwenye jamii forum :http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/296767-sheria-mpya-ya-mafao-haiwagusi-wabunge-na-viongozi-wengine-wakubwa.html

hatarisho:habari hii haina uthibitisho...japo lisemwalo lipo...kama halipo laja

1 comment:

  1. kama ni kura ..nakataa kabisa...sijui wenzangu kama mnaona ni sawa

    ReplyDelete