Friday, July 27, 2012

CHUO CHA SAME KIKO HATARINI KUINGILIWA NA WANYAMA WAKALI


Chuo cha maendeleo ya wananchi wilayani Same mkoani  Kilimanjaro kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio hali ambayo imekuwa ikisababisha wanyama kuingia ndani ya chuo hicho nakuhatarisha usalama wa wanafunzi katika chuo hicho. Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo hicho Bi Theresia Mianga alipokuwa akizungumza  na waandishiwa habari juu ya changamoto zinazokikabili chuo hicho kwa kipindi cha muda mrefu tangu kuanzishwa kwa chuo hicho ambacho hakijawahi kuwa na uzio hadi sasa.


Amesema kuwa kukosekana kwa uzio katika chuo hicho kumesababisha wanyama wanaotoka katika hifadhi ya Taifa ya Mkoazi kuingia chuoni hapoa kwa urahisi. Amesema kuwa ni vyema Serikali inapaswa kuweka uzio katika chuo hicho ili kuweza kudhibiti wanyama wa hifadhi hiyo kuingia katika chuoni hapo,ili waalimu,wanafunzi na wafanyakazi wakaishi kwa usalama.

Aidha ameongeza kuwa changamoto nyingine inatokana na ukosefu wa uzio katika chuo hicho ni pamoja na usalama wa mali za chuoni hapo kuibiwa na watu kutokana na maeneo ya chuo hicho kuwa  wazi.Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Salumu Wiliamu alisema kuwa ukosefu wa uzio katika chuo hicho kumesababisha kuwepo na wanyama wanaingia kutoka hifadhi mkomazi na kuingia katika maeneo ya shule hapo.

Kwa upande wake mkufunzi wa chuo hicho Bw Cathbert Msuya alisema kuwa chuo hicho kimeweza kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali hapa nchini kutokana na elimu inayotolewa chuoni hapo.Aidha alitoa wito kwa vijana hapa nchini kujiunga na vyuo vya maendeleo ya jamii ili waondokane na tatizo sugu la umasikini linalowakabili watu wengi kwa sasa hapa nchini.
   

No comments:

Post a Comment