Friday, July 27, 2012

SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI IMEZUA MGOGORO BUNGENI


Mbunge wa Mwibara, mkoani Mara, Bw.Kangi Lugola (CCM),amewalipua wabunge waliopitisha sheria kandamizi ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii na kurejea kauli yake kuwa chombo hicho hakiko makini katika kutunga na kupitisha sheria

Bw. Lugoda alitoa tuhuma hizo bungeni mjini Dodoma baada ya kuomba muongozo wa spika wa kutokana na hatua ya Mbunge wa Kisarawe, Bw. Suleiman Jaffo(CCM)kuomba muongozo wa kulitaka Bunge hilo lisitishe shughuri zake ili kujadili hoja ya dharura ya malalamiko makubwa yanayotolewa na wananchi kuhusu sheria hiyo

Baada ya kuruhusiwa kuzungumza Bw. Jaffo alisema sheria hiyo ni kandamizi ambapo mfanyakazi hawezi kupata mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 55 hadi 60 ,alisema kuwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali hivyo kulitaka bunge liahirishe shughuri za siku hiyo na kujadilinkwa dharula hoja hiyo

Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, na Bw. Tundu Lissu walitaka itishwe kamati ya uongozi kujadili jambo hilo lenye madhara makubwa kwa wafanyakazi, kutokana na hali hiyo Bw. Lugoda aliomba muongoza na kueleza kuwa suala hilo ni la kisheria na wabunge wabunge wanapolalamikia sheria hiyo ni wazi kuwa Bunge haliko makini kwenye kutunga na kupitisha sheria zake

Baada ya marumbano makubwa Bi. Mhagama aliagiza kikao cha kamati ya Uongozi ya Bunge ikutane ili kujadili suala hilo kuona ni namna gani Bunge linaweza kusaidia na kuifanya marekebisho

No comments:

Post a Comment