Tuesday, June 19, 2012

MFUMO MPYA WA MAWASILIANO UMEINGIA SOKONI



Taasisi Makampuni na Mashirika ya umma nchini yameshauriwa kujiunga na teknolojia mpya ya mawasiliano ya simu za mezani zenye uwezo wa kukutanisha zaidi ya watu wawili wakiwa maeneo tofauti huku wakionana.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Sihebs Technologies Company Ltd katika ofisi zao zilizopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, Bi.Rachel Israel wakati akizungumzia simu hizo zenye uwezo mkubwa katika mawasiliano. Alisema simu hizo ambazo zinatumia mtandano wa intaneti ziko katika mfumo wa video ambao huwafanya wanaozungumza kuonana uso kwa uso katika mazungumzo yao.

Bi.Rachel alisema pia mfumo huo unawezesha mawasiliano kuwa rahisi na kuokoa muda katika shughuli za kukuza uchumi. “Teknolojia hii ni mpya kabisa hapa nchini na sisi ndiyo watu wa kwanza kuiingiza sokoni,ni teknolojia ambayo ina faida nyingi kwanza kabisa inaokoa muda,watu hata wakiwa nje ya mikoa wanaweza kuzungumza na kuonana katika kioo (screen) kilichopo katika simu hiyo,”alisema Bi.Rachel.

Alisema faida nyingine ni kuokoa matumizi ya fedha,kurahisisha huduma kwa wateja kwa zile kampuni ambazo zinatoa huduma kwa wateja. “Mfumo huu unasaidia kuokoa karibu asilimia 90 au zaidi ya gharama za mawasiliano katika kampuni au shirika,lakini pia hautiji kuwa na mlolongo wa kusubiri kuunganishwa na opareta,ni simu ambayo watu wanaunganishana moja kwa moja,kinachohitajika ni kutengeneza mtandao wa ndani wa mawasiliano,”alisema Bi.Rachel.

Alisema tayari mfumo huo umeshaingia sokoni na tayari baadhi ya kampuni zimeshaanza kuutumia kwa ajili ya shughuli za kiuchumi. Wito wangu ni kwamba katika kipindi hiki ambacho nchi inatakiwa kuzalisha zaidi basi ni vizuri kampuni na hata taasisi za umma zikatumia mfumo huu nafuu na wa haraka zaidi,watumiaji wataokoa muda kwa kutumia teknolojia hii mpya,”alisema Bi.Rachel.

Mbali na kufunga mitandao kampuni hiyo pia hufanya ushauri kuhusiana na suala zima la mitandao,kufunga vifaa na ukarabati wa mitandao ya mawasiliano.






No comments:

Post a Comment