Saturday, June 23, 2012

UONGO WA LULU ULILENGA KUIPA HADHI FILAMU


Mama mzazi wa msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' Lucresia
Kalugila, amedai kitendo cha mwanawe kutamka mbele ya umma kwamba
anaumri zaidi ya miaka 18, kililenga kuipa hadhi filamu yake


Alidai pia kwamba mtoto huyo alifanya hivyo ili kuepuka unyanyapaa
ambao ulikuwa ukifanywa dhidi yake na wasanii wenzake katika sanaa ya
filamu wakimueleza kuwa ni mtoto

Lucresia alidai hayo kupitia hati ya kiapo ya majibu aliyowasilisha
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam akikana mwanawe kuwa na umri wa
zaidi ya miaka 18

Hati hiyo ya majibu iliwasilishwa jana Mahakamani hapo mbele ya Jaji
Dk. Fauz Twaib na mawakili Kenneth Fungamtama, Peter Kibatala pamoja
na Fulgence Massawe wanaomwakilisha Lulu

Mawakili hao waliwasilisha hati hiyo ya majibu baada ya Jamhuri
kuwasilisha ushahidi wa CD ya mahojiano ya Lulu na mtangazaji Zamaradi
Mketema, maelezo yake aliyoyatoa polisi maombi ya hati ya kusafiria
pamoja na leseni ya udereva

Katika ushahidi huo wa jamhuri inaonekana muombaji wa kufanyiwa
uchunguzi kuhusu utata wa umri wake akisema anaumri zaidi ya 18

Mama huyo amedai kwamba anaamini kuwa Lulu kutokana na utoto wake
alitoa matamko ya uongo ili aweze kupata hati ya kusafiria na leseni
ya udereva na kwamba si kweli amezaliwa Aprili 17, mwaka 1991 kama
alivyoeleza

No comments:

Post a Comment