Friday, June 22, 2012

TUBORESHE KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Sadick Meck Sadick amesema kuwa ili tuondokane na upungufu wa njaa ni lazima tuendeleze kilimo cha umwagiliaji kwa kuboresha miundombinu . Aliyasema hayo alipokuwa akifunga maonyesho ya kilimo cha mpunga yaliyofanyika Jijiji Daresalaam.


Alisema kuwa, miundombinu inayotakiwa kuboreshwa ni skimu za umwagiliaji pamoja na kuboresha miundo mbinu ya zamani ili wakulima wapate mazao yatakayoleta tija kwenye masoko ya ndani ya Nchi na nje ya Nchi.

Hata hivyo alisema kuwa, Serikali,wadau na wafadhili mbalimbali Nchini wanatakiwa kuwekeza katika kilimo hicho ili kuwawezesha Wananchi kuondokana na hali ya utegemezi pamoja na kuinua pato la Taifa.

``Ukweli usipopingika, ili tuondokanea na upugufu wa njaa ni lazima Serikali,wafadhili mbalimbali Nchini,pamoja na maafisa ugani kuboresha miundo mbinu ya kilimo hiki``alisema,Bw Sadick.

Alitoa mwito, kwa Wakulima Nchini kuuza mazao yao kwa kufuata madaraja ya bei ili wapate faida pale wanapoyapeleka kwenye masoko.


No comments:

Post a Comment