Kituo cha
Kimataifa cha Anga za Juu, maarufu kama 'International Space Station' (ISS),
wiki hii kimeonekana kuwa katika hatari ya kugongwa na vyombo vinavyopeleka
huduma kwa wanaanga wanaoishi ndani yake huko angani.
Uwezekano huo unatokana na chombo cha anga cha Urusi ambacho kilipeleka
mahitaji kwa wanaanga hao, kushindwa kutia nanga kituoni hapo katika operesheni
ya kujaribu mbinu mpya ya kutia nanga badala ya iliyozoeleka.Sababu ya kufanya hivyo ni kutaka kubuni mkakati bora zaidi wa kuwezesha
vyombo visivyo na rubani kuongozwa kutokea duniani mpaka kwenye kituo hicho na
kutua kwa urahisi, hususan katika safari zijazo.
Tunaposema kutia nanga, maana yake kwa lugha nyingine ni
"docking", yaani chombo cha anga kutoka duniani kujiunganisha na
kituo hicho kama ifanyavyo meli inapowasili bandarini na kujiunganisha na gati
ya bandari ili kuwezesha abiria kuteremka au kupakuliwa shehena ya mizigo.
Ni kama vile meli inavyowasili banadarini na kutia nanga, ambapo hufungwa kwa kamba maalumu ili mawimbi ya maji yasiisogeze kutoka mahali pake mpaka unapowadia muda wake wa kuondoka.
Zana ambazo hupelekwa katika kituoni hicho ni vipuri, pamoja na vifaa vya majaribio ya kisayansi na huduma ya vyakula kwa ajili ya wanaanga.

Chombo hicho cha Urusi kiitwacho 'Progess 47' kilirushwa kutoka duniani
Aprili 20 mwaka huu na kiliwasili kituoni hapo na kufanikiwa kujiunganisha,
ambapo kiliendelea kubaki hapo mpaka Jumapili iliyopita kilipojiondoa na kwenda
umbali wa kilometa 160 kutoka kituo hicho ili kurejea na kujaribu kujiunganisha
tena kwa kutumia hiyo mbinu mpya.Ni katika operesheni hiyo ambapo chombo hicho kilijaribu mara mbili
kutia nanga na kushidikana. Chombo hicho cha Russia kinatarajiwa kujaribu tena
operesheni hiyo leo Jumapili Julai 29, 2012.
Wasi wa waratibu wa shughuli za kituo hicho ni kwamba inaweza ikatokea siku moja chombo kikashindwa kujiegesha katika 'gati' na kukigonga kituo hicho, au chombo kushindwa kutia nanga wakati kinawapeka wanaanga wapya kituoni na kuwachukua waliopo ili kuwarejesha duniani.
Wahandisi wa Russia wamekaririwa na gazeti la 'The Moscow Times' wakisema kwamba hitilafu iliyojitokeza si ya kuhatarisha kituo hicho.
Kituo hicho huelea angani taratibu kutokea Mashariki kuelekea Magharibi, kupingana na uelekeo wa dunia ambayo hujizungusha yenyewe kutoka Magharibi kwenda Mashariki.
Umbali kutoka duniani mpaka kilipo kituo hicho ni wastani wa kilometa 370, lakini pia wakati mwingine umbali huo huongezeka mpaka kuwa kilometa 405 hivi.
Uzito wa kituo hicho cha kimataifa ni kilo 450,000 (tani 450), urefu meta 73, upana meta 109, na kimo meta 20.
Kutokana na vipimo hivyo, kituo hicho hushuka taratibu kuelekea duniani kwa takribani kilometa 2 kila mwezi.
Ukubwa wa ndani, ambamo kuna vyumba kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za kisayansi, ni sawa na wa ndege kubwa ya abiria ya aina ya Boeing 747, maarufu kama 'Jumbo Jet' ambayo ina uwezo wa kubeba watu 540.
Aina hiyo ya ndege husafiri masafa marefu bila kutua, na ni ile ambayo kwa upande wake wa mbele ina kigorofa.
Kwa faida yako Msomaji ni kwamba umbali kutoka mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini, mpaka Sydney, Australia, ni kilometa 11,105 za anga, ambapo ndege hiyo kuzichana ikiwa juu ya Bahari Kuu ya Hindi kwa saa 13 bila kutua popote.
Kwa upande wa kituo hicho cha anga, ni kwamba kina uwezo wa kuhudumia kwa mara moja wanaanga 7, lakini, hata hivyo, chaweza kumudu kutoa huduma kwa watu zaidi kama ilivyotokea Julai 2009 ambapo wanaanga 13 waliweza kuishi kituoni hapo kwa siku 11.
Baadhi ya wanaanga walikuwa wakilala kwenye chombo chao cha anga, ambacho muda wote kiliendelea kutia nanga kituoni hapo.
Kituo hicho kimeundwa kwa utaalamu wa hali ya juu, ambapo umeme unaotumika ni wa mwanga wa jua (solar) ambao hunaswa na mbawa (pannels) ndefu na fupi zenye madini ya kunasa mwanga huo na kuugeuza kuwa nishati ya umeme.
Mbawa hizo zimepangwa kuelekea pande zote, yaani juu, chini, na pande nne za dunia, ili kunasa kiasi kingi cha mawimbi.
Mbawa ndefu kuliko zote ina urefu wa meta 40, ambapo zote kwa pamoja huweza kutoa nishati ya kilowati 84 ambazo ni tosha kukifanya kituo kujiendesha bila umeme kukatika kama ilivyo hapa duniani.
Kuna vyumba viwili, choo mbili, chumba cha kufanyia mazoezi ya viungo, maambara mbili, na ukumbi wa maongezi.
Vyumba katika kituo hicho vina madirisha ya vioo yasiyofuguka, bila kusahau kuwa wanaanga wanapo kuwa ndani ya kituo hicho hawahitajiki kuvaa yale mavazi yao mazito ya anga bali huwa katika zare zao za kawaida za kikazi.
Kutofunguka kwa madirisha ni mojawapo ya sharti kuu la safari za anga, ambapo hewa ya oksijeni tunayoitumia ili kuwa hai haitakiwi kuchanaganyika na hewa zilizopo huko anga za juu kwa kuwa ni za sumu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA), ni kwamba unapokuwa kwenye kituo hicho cha anga na kuiangalia dunia kwa chini, takribani asilimia 85 ya eneo lote la dunia huonekana, na pia asilimia 95 ya makazi ya binadamu, ikiwemo miji, vijiji, na kadhalika, huweza kuonekana kwa kupitia kiona mbali.
Wanasayansi wanaoshughulika na chombo hicho wanakadiria kuwa ifikapo mwaka 2016 au 2020 kituo hicho hakitafaa tena kuendelea kufanyakazi yake vyema, na hivyo kitaharibiwa kwa namna ambayo hakitaleta athari kwa mazingira ya dunia.
Wanaanga walianza kuishi kituoni hapo tangu Novemba 2, 2000, na wamekuwa wakipeana zamu na wenzao kutoka duniani mara kwa mara.
Hii ikiwa na maana inapoonekana kwamba kuna hitaji la kufanyika uchunguzi wa kitu chochote cha kisayansi katika mazingira ya anga, iwe ni uchunguzi wa kibaolojia, fizikia, kemia, au chochote kile muhimu, basi mhusika hupewa nafasi ya kwenda kufanya utafiti wake huko anga za juu na kurejea duniani akiwa na majibu.
Wazo la kuwa na kituo hicho huko angani lilitolewa mwaka 1984 na Rais wa zamani wa Marekani, Bw Ronald Reagan, ambaye aliwaambia wananchi wake kwamba kulikuwa na umuhimu wa taifa lao kuwa na kituo cha kudumu huko anga za juu kwa lengo la kuichunguza anga na dunia kwa wakati mmoja.
Mwaka 1991, serikali ya Rais George Bush (sio Bush-mtoto) ilikubaliana kwa mapatano maalumu na Rais Makhail Gorbachev wa Urusi ili nchi zao ziendeshe kituo hicho kwa ubia, lakini chini ya uratibu wa NASA.
Nchi nyingine zenye ubia wa kituo hicho ni Uingereza, Japani, Ufaransa, Kanada, Uhispania,Ubelgiji, na Ujerumani.
Nyingine ni Brazili, Denmark, Norway, Swedeni, Uswiss, Italia, na Uholanzi, ambapo wakati huu kuna wanaanga 6 ndani ya kituo hicho ambao ni mmoja kutoka Japani, wawili ni Wamarekani, na Warusi watatu.
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, vyombo vitatu vya anga vya Marekani, viitwavyo 'Space Shuttle', ndivyo vilikuwa vikisomba kwa zamu zana za ujenzi kwenda huko angani katika kazi ambayo ilikuwa ni ngumu na mojawapo ya hatari kufanywa na binadamu huko anga za juu.
Vyombo hivyo ni Atlantis, Discovery, na Enterprise, ambapo Challenger cha nne kilipata ajali wakati kikiondoka duniani kwenda huko na kuua wanaanga wake 7.
Columbia ni chombo kingine kilicholipuka angani na kuua wanaanga wengine 7 wakati kikipita katika eneo la anga lenye joto kali kureja duniani. Hiyo ilikuwa Februari 7, 2003.

No comments:
Post a Comment