Saturday, June 23, 2012

SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI LIMECHUKUA SURA MPYA


SAKATA la mgomo wa madaktari nchini limeendelea kushika sura mpya
baada ya mgomo huo kuanza kwa chini chini katika baadhi ya hospitali.Timu ya waandishi lilizunguka katika baadhi ya hospitalini nchini na kubaini kuwepo kwa mapungufu ya huduma za hospitali.


Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),wagonjwa waliendelea
kupokelewa kama kawaida lakini hawakuweza kupata huduma za madaktari.Waandishi walitembelea baadhi ya wodi hospitalini hapo na kubaini kuwepo kwa mgomo baridi kutokana na wagonjwa kutopata huduma kwa wagonjwa.

Katika wodi ya Kibasila baadhi ya wagonjwa waliozungumza na gazeti
hili walieleza kuwa, tangu jana asubuhi hakukuwa na madaktari
waliowapitia wagonjwa hali ambayo wamebaini kuwepo kwa mgomo wa
kichini chini.

Mgonjwa mmoja aliyelazwa katika wodi ya Kibasila (jina tunalo)alidai kuwa jana ilikuwa ni siku yake ya kufanyiwa upasuaji lakini hakuweza kufanyiwa kwa sababu asizozijua. "Jana nilitakiwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo lakini hadi muda huu wa jioni hakuna maandalizi yoyote na sijamwona daktari yoyote akipita
wodini au hata kupewa maelekezo kabla ya kwenda kufanyiwa, " alisema.

Hali hiyo ya madaktari kutopita katika wodi hizo pia ilijitokeza katika wodi za Sewahaji na Mwaisela ambapo wagonjwa kutopata huduma kutoka kwa madaktari bingwa. Katika Hospitali ya Temeke, hali ya kutolewa huduma ilikuwa ikiendelea kama kawaida isipokuwa kulikuwa na hali ya mgomo wa chini chini wa
madaktari (Medical doctor).

Akizungumzia hali ya mgomo huo mmoja wa viongozi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lakekuandikwa, alisema kuwa huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida na wagonjwa wanaendelea kupokelewa sipokuwa madaktari wamekuwa hawapatikani.

Alisema kutokana na hali hiyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi umegundua kuwa baadhi ya madaktari wameanza mgomo wa chini chini kwani hakukuwana daktari hata mmoja aliyeweza kuzungumzia suala hilo hata walipotafutwa kwa njia za simu waliahidi kuzungumza.

Katika hospitali ya Amana baadhi ya manesi waliozungumza na Mwandishi wa habari hizi walidai kuwa mgomo hakuna isipokuwa mdaktari hawaonekani lakini huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida.

Hata hivyo baadhi ya madaktari wa ngazi za chini waliozungumza na mwandishi wa habari hizi ambao hawakupenda majina yao kuandikwa, walidai kuwa hawatoweza kushiriki katika mgomo huo kwa kuwa wanaofaidika ni madaktari bingwa.

"Sisi tumekubaliana tuendelee na kazi nadhani mmepita katika hospitali zingine, kwani hata tukishiriki wanaofaidika ni wenzetu hivyo hakuna sababu, " alisema.

Katika Hospitali ya Mwananyamala kulikuwa na manesi waliokuwa wakiendelea na kutoa huduma kwa wagonjwa lakini idadi ya madaktari waliokuwepo ilikuwa ndogo.
"Usiniandike  mimi sio msemaji, kweli baadhi ya mdaktarihawapo sasa hatujui kama tayari wameanza mgomo ama la na ukizingatia leo ni siku ya mapumnziko hivyo siku nzuri ni Jumatatu ambayo ni siku
ya kazi, " alisema.

Hata hivyo waandishi wa gazeti hili walitembelea katika wodi ya
wajawazito na watoto lakini hakukuwa na huduma, licha ya kuwepo kwa
mgonjwa mmoja aliyegongwa na gari na kujeruhiwa vibaya lakini hakuweza
kupata huduma kwa haraka.

Waandishi waliamua kuwatafuta baadhi ya viongozi wa madaktari na
kuwathibitishia kuwa wanaandaa maelezo ya kuijibu Serikali ."Tusubirini kidogo tunaandaa (stement) maelezo ya kuijibu Serikali hivyo hadi saa saba tunatarajia kuzungumza na waandishi, " alisema
kiongozi mmoja wa madaktari hao.

Hata hivyo waandishi walisuburi hadi kufikia muda wa saa tisa jioni lakini hakukuwa na majibu na hata walipofuatwa kwenye eneo la mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco kama walivyodai lakini hawakuwepo na badala yake kulikuwa na shughuli zingine katika ukumbi huo.


  Mwandishi wa habari hii ilifanya mawasiliano na ofisa habari msadizi wa hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)ambaye alikataa kuzungumzia hali hiyo na badala yake alisema kuwa yupo bosi wake ambaye ni Aminieli Aligeisha na kuwataka waandishi kumsubiri ili azungumzie ambapo hadi kufikia majira
ya saa tisa kasoro jioni alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya kiganjani

No comments:

Post a Comment