Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Adbdul
‘Diamond’ anatarajia kupamba mashindano ya kumsaka Redd's Miss Dar Intercollege
2012, yaliyopangwa kufanyika Juni 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa , uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa mashindano hayo
Dina Ismail alisema mbali na Diamond, onesho hilo pia litapambwa na burudani
kutoka bendi ya Skylight ambayo ipo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame
mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema maandalizi yanakwenda vyema ambapo warembo 14,
watakaosghiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tumejipanga vyema kuhakikisha mmoja ya warembo
kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vizuri katika fainali za Miss Tanzania,”
alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki mashindano hayo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa
Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT ambapo taji hilo linashikiliwa na Rose
Msuya kutoka IFM.
Dina aliwataja wanyange watakaopanda jukwaani kuwa ni
Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica
Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose
Masanja na Jamila Hassan.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kupitia bia yake ya Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,
Lamada Hotel na Screen Masters.
Wengine ni Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear
Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Spoti Kizaa zaa na blog za Michuzi,
Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.
ends.......
No comments:
Post a Comment