Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili msanii Elizabert Michael 'Lulu'umewasilishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ushahidi wake kuhusu utata wa umri wa msanii huyo
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mahakamani hapo ushahidi huo uliwasilishwa jana ambapo miongoni mwa ushahidi CD ya mahojiano kati ya Lulu na mtangazaji wa Luninga ya Clouds TV,Zamaradi Mtetema
Ushahidi mwingine ni maelezo ya polisi yaliyotolewa na msanii huyo, fomu za maombi ya hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari, ilielezwa kuwa katika ushahidi huo unaonyesha Lulu akisema ana miaka 18
Baadhi ya mawakili wanaomtetea Lulu katika kesi hiyo Pete Kibatala, Flugency Massawe ambapo katika ushahidi wao waliwasilisha hati ya kiapo cha wazazi wa msanii huyo
Jalada la kesi hiyo kwa sasa lipo Mahakama Kuu mbele ya Jaji Dkt.l Fauz Twaib, anayesikiliza madai ya utata wa umri wa msanii huyo ambapo uwamuzi wa utata huo unatarajiwa kutolewa Juni 25 mwaka huu
Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba Aprili 7, mwaka huu anadaiwa kuwa chini ya miaka 18 huku Jamuhuri ikidai kwamba mshitakiwa huyo ana zaidi ya umri huo
No comments:
Post a Comment