Wednesday, June 20, 2012

WATOTO WANANAFASI KUBWA KATIKA FAMILIA

WATOTO katika familia wana raha  pale tu wanapopata malezi bora kutoka kwa wazazi wao hasa wakiwepo wote wawili baba na mama

Wataalamu mbalimbali duniani wameorodhesha hatua kama nne katika makuzi mbalimbali ya mtoto ikiwemo ya mtoto kula chochote anachoshika mkononi,kujisaidia na kumpenda sana mzazi mmoja wapo ambapo anaweza kuwa baba ama mama


Katika hatua ambazo watalaamu wa saikoilojia waliamua kuchambua kimojawapo ambacho kimekuwa kikiwapa shida sana jamii pale wanapoona mtoto akiwa na umri mkubwa akipenda sana kuwa na urafiki na watu wa jinsia tofauti na yeye

Inasemekana kuwa mtoto anapompenda mzazi wake mmoja huendelea na tabia hiyo hadi ukubwani ambako kama ni mtoto wa kike amempenda baba yake basi ukubwani kwake marafiki zake wakubwa watakuwa ni wanaume tu na kila utapomkuta basi asilimia 99 utamkuta na wanaume

Pamoja na hilo pia hata mavazi yake yatakuwa ni ya kiume kwani kuvaa sketi,blauzi,ama hata magauni kwake ni mwiko kabisa na siku ukimuona amevaa gauni basi ujue siku hiyo ni mgonjwa ambaye hawezi hata kuinuka hivyo gauni hilo amevalishwa kwa kuwa hajiwezi

Watoto wa namna hii hujisikia faraja sana kwa kuwa na watu wa jinsia tofauti na yeye kwa kuwa tokea utoto wake amekuwa karibu sana na baba yake na kumpenda kuliko mama yake na mara nyingine hufikia hata kuwagombanisha wazazi wake kwa kuwa mtoto anaweza kuonesha upendo wa wazi kati ya mama na baba yake

Kwa upande wa watoto wa kiume ambao katika makuzi yao humpenda sana mama kuliko baba basi na wao wanapofika ukubwani kupendelea kuwa na marafiki wengi wa kike kuliko wa jinsia yake ya kiume

Watoto hawa huvaa mavazi ya kawaida ya wanaume lakini kila utakapomuona yuko na mwanamke sehemu zote na kama anasoma basi ndio usiseme ukimuona kwenye kundi la wanaume wenzake basi kuna kazi wanafanya ambayo ni ya pamoja

Hapo ndipo wazazi wanapoanza kuisi hivi ni kwanini mtoto wangu anapenda kuwakaa na wanawake ikiwa yeye ni wa kiume ambapo watoto hawa hapenda kushinda na mama zao wawapo nyumbani hata siku nzima ambapo mama na mwanaye wa kiume wanaweza wakaongea mambo mengi tofauti na mtoto wa kiume ambavyo angetakiwa kuongea na baba yake

Watoto hawa huweza hata kufanya kazi za ndani bila kinyongo hata kama dada zake wapo ingawa si kosa kufanya hivyo lakini kwa jinsi jamii ilivyo inaweza kuwa tatizo kuona mtoto wa kiume akipika,kufua nguo ikiwemo vitambaa vya kutandika kwenye makochi,kupiga deki,na kufagia uwanja ambapo mara nyingi wamekuwa wakifanya watoto wa kike kazi hizo

Katika hatua kama hizo wapo vijana katika jamii ambao wanahisi kuwa labda kazaliwa tofauti lakini si hivyo bali ni hali tu inayoweza kujitokeza kwa mtoto anapokuwa mdogo hadi mkubwa akiwa anapenda sana marafiki walio tofauti na jinsia yake

Kwa hakuna ubishi na si dhani kama kuna mtu anweza kupinga kuwa hakuna watu wa jamii hiyo aliowahi kuwaona katika maisha yake labda awe mtoto lakini ni kijana ama mzee utakuwa umewaona

Watoto hawa ambao huwa hivyo ni vigumu sana kuwabadilisha kwa kuwa ndivyo saikolojia yao inavyoamini kuwa marafiki alionao ndio sehemu ya kufurahia maisha yake

Lakini pamoja na hayo wapo watoto ambao wao huwa na upendo kwa baba na mama ambapo wao huwa hawawezi kuonesha kuwa kati ya baba na mama wote ni bora kwake hivyo kwa jinsi wanavyokuwa wanaendelea kuwa na upendo kwa wazazi wao wote wawili hata kama baba na mama yake walitengana lakini wao huendelea kuwa na upendo na wazazi wao

Kwa hali hiyo wazazi wanatakiwa kuwachunguza watoto wao mapema na pindi wanapogundua kuwa mtoto ana upendo na mzazi moja basi ni vizuri kuhakikisha kuwa anatengenezewa mazingira ya kuwapenda wote lakini hiyo ikishindikana basi ujue kabisa atakapokuwa mkubwa hataweza kukuthamini wewe mzazi ambaye alikuchukia tangu akiwa mdogo

Saikolojia yake ikisha komaa kwa kuamini baba ama mama ndio mtu bora kwake hata ufanyeje hutaweza kuibadili kwa kuwa yeye anaamini hivyo na ataendelea kuamini hivyo

  Mwandishi; Goodluck Hongo


No comments:

Post a Comment