Mara nyingi hutumika kwa ajili ya
mafundisho ya ndoa kwa mtoto wa kike anayetarajiwa kuolewa au kuishi na mume, Wanapewa
mafunzo ya ndoa na mapenzi kwenye mikusanyiko inayoitwa "kitchen
Parties". Mwanafunzi huyo
anatarajia kupata vingi vipya ikiwemo na viombo vya ndani hususani vya jikoni Katika
mafunzo hayo wanaambiwa mambo ya mapenzi na hususan jinsi ya kufanya mambo
fulani fulani na kuhusiana na mwenza. Matarajio ya mafundisho hayo ambayo
hukusanya wanawake wengi ni kuwa mfundwa (kama tunaweza kuita huko ni kufundwa)
ni kwamba atakuwa amejiandaa kwa maisha ya ndoa na mapenzi.
Kitchen Parties kimsingi imechukua nafasi ya utamaduni wa unyago ambapo wamama watu wazima ambao wanaheshima katika jamii hutoa mafunzo ya maisha ya ndoa kwa mabinti mara kwa mara (kama siyo mara zote) ni mabikira au ambao hawajawa katika mahusiano ya muda mrefu (wachanga wa mapenzi). Unyago uliongozwa na wale tuliowaita Makungwi. Siri za unyago kwa wamama zetu ni siri wanazoenda nazo kaburini. Mambo ya KP yamekuwa ni gumzo na yanarekodiwa kwenye video siku hizi.
Miaka hii michache iliyopita dada zetu na wadogo zetu wamepelekwa huko (au wamejipeleka wenyewe) na kufanyiwa hizo kitchen parties. Kwa upande wetu sisi wanaume sijui kama tumefaidika na mafunzo hayo au ndio tumepata ubutu wa kisu cha kina dada kujua kuwa na "vidumu" au kuwa promiscuous au kutojali mapenzi ya mume.
Hata hivyo ninabakia kujiuluiza kama maisha ya ndoa na mahusiano kati ya mume na mke yamejengwa au kufaidika na haya mambo ya KP au ni bora njia bora ya kutumia wamama watu wazima kufundisha mambo haya? Ni mama gani leo ambao ana ujuzi wa mambo ya mapenzi kama hawa vijana? Sehemu nyingine tumeona kuwa KPs inahusiana na mambo ya ngono zaidi kuliko mahusiano ya wapendanao kiasi kwamba wadogo zetu na dada zetu wanafikiria mahusiano ya ndoa ni mambo ya ngono tu.
Kitchen parties ni sehemu ya suluhisho ya matatizo ya ndoa au ni sehemu ya tatizo?
No comments:
Post a Comment