Friday, August 3, 2012

TUJITAHIDI KUONGEZA WASHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Kwa uchanganuzi uliofanywa na blog views, umeona kuwa Tanzania ingepaswa kuwa na washiriki zaidi ya Nchi jirani kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea Mjini London hivi sasa, kutokana na hali nzuri ya kisiasa na mahusiano yake kimataifa.



Idadi ya washiriki kwa Afrika mashariki

Rwanda ina jumla ya washiriki 7, wakiwemo waogeleaji 2, wakimbiaji 3,judo 1, na mwendesha baiskeli 1

Kenya ina jumla ya washriki 50,wakimbiaji 45,ndondi 2,waogeleaji 2, na mnyanyua vitu vizito 1

Burundi ina wasiriki 6 , wakiwemo waogeleaji 2,wakimbiaji 3 na judo 1

Tanzania ina jumla ya washiriki 7, wakiwemo waogeleaji 2, wakimbiaji 4, na ndondi 1,

Uganda ina washiriki 16, wakiwemo wakimbiaji 12, waogeleaji 2,myanyua vitu vizito 1, na mchezo wa kinyoya 1

Swali ni kwamba, kwa nini tushindwe kupeleka wanamichezo mbalimbali kwenye mashindano ya kimataifa.
Wizara, pamoja na  wahusika katika michezo tunafanya nini kuweka umuhimu kwenye michezo na kupata matokeo mazuri kwenye mashindano mbalimbali.

Je? hatuna wachezaji wenye uwezo wa kufundishwa wakawa washindani kimataifa?

Hili ni jukumu la watanzania kuonesha kukerwa kwetu kwa kuwa nyuma kimichezo, kaiasi kwamba, hata nchi jirani zimeanza kuwa na mwelekeo wa kufanya vema zaidi kuliko Tanzania.

No comments:

Post a Comment