Saturday, August 11, 2012

MAKOSA YANAYOFANYWA NA MABINTI WAINGIAPO KWENYE MAHUSIANO


Makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua nani wa kumuoa ,kuolewa ni swala la makubaliano kati ya watu wawili wenye jinsia tofauti .Katika harakati za kuolewa kuna masuala mengi ya kuangalia ili binti asifanye kosa wakati wa kuchagua mtu wa kumuoa , kosa kwa binti anayetaka kuolewa ni kama ifuatazo

Kuamua kuolewa na mtu ambaye ni mkorofi , ukiwa na mayawo kuwa ataweza kubadilika akiwa ndani ya ndoa , ni vigumu sana mwanaume kuondoa dosari zake wakati akiwa ndani ya ndoa tena mbali na hiyo atazidisha dosari .Kama wewe unatarajia kuolewa hivi karibuni kuwa makini na neon ‘I LOVE YOU’ kuna wanasakolojia wanaeleza kuwa hilo neon maana yake ni ‘NINA UCHU NAWE’ kwani asilimia kubwa wanatamani mwili na hawana kitu kingine mbali na mapenzi

Lazima uangalie mume wako ni mtu wa kusamehe au kulipiza kisasi kwa maadui anatoa msamaha kwa masikini ni mwaminifu, anachosema ndicho anachotekeleza au ni longolongo mpaka mwisho, ni mbabaishaji anamajungu mengi, anajipenda ni mchafu, au hana mpangilio wa maisha yanaendaje, anayajua mapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba kila mara

Akishauriwa na ndugu na marafiki zake yupoteyari au anakuja na maamuzi yasiyo na msingi wa maendeleo bila ya kujitambua , watafiti wanasema ni heri kuolewa na mwanaume ambaye upon ye katika fani moja kwani ni rahisi kutambua udhaifu wake na uwezo wake katika maisha yenu, kama ni mwalimu basi mtafute mwali, ingawa hili si lalazima sana

Swala kubwa na muhimu unaamua kuolewa na mtu amabaye ushawahi kukutana naye kimwili bila ndoa na haujawahi kufanya tafiti ya kutosha unauwezo wa kusababisha matatizo yasiyo na mwisho, Tendo la kukutana kimwili kabla ya ndoa linafunika uwezo wa mtu kufikiri kwani mtu atawaza ngono na ubongo utatawaliwa na masuala hayo na kushindwa kufikiria masuala mengi ya maisha

Binti unaolewa na mtu amabaye hata ukimuona haupati msisimko wa mwili yaani hakuvutii kimapenzi mwanamke anaweza akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya gari analomiliki , hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutiwa na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo

Usikubali kuolewa na mwanaume anayekudhibiti kwani ni kwa faida yake ni kheri kuolewa na mwanaume mabaye anakupa mawazo kwani ni kwa faida yako na si vinginevyo,

Binti najuta baada ya kuolewa kwa kukimbia matatizo aliyo nayo yumbani kwake hapo si sahihi kani hapo anajiongezea matatizo utampata bwana na kahara juu na utajuta kuolewa naye.

Usiolewa na mtu anayetawaliwa ‘Hobbie’ wala hawategemei wazazi mtu mabaye ni mrevi wa pombe au dawa za kurevya anayependa fedha bila ya kufanya kazi anayependa mpira au michezo, lazima wote muwe na muda wa pamoja wa kukaa na kushauriana masuala mbalimbali ya kimaendeleo







No comments:

Post a Comment