*Watangaza kumtenga msajili vyama vya siasa *Wataka tume huru, waiweka serikali mtegoni
Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tume hiyo itasaidia kubaini ukweli wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi ili wahusika wachukuliwe hatua na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika kisiasa kukisingizia chama hicho kuwa ndio kinara cha mauaji ya raia katika mikutano yao.
“Katika kikao chetu cha Kamati Kuu, tuliazimia kumtaaka Rais Kikwete aunde tume huru kuchunguza mauaji ya raia, pia tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema na Mkuu wa Oparesheni Makao Makuu ya jeshi hili, Bw. Paul Chagonja wajiuzulu.
“Pia tunamtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro na Iringa wakiwemo na Makamanda wa Vikosi vya FFU katika mikoa hii, wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji,” alisema.
Alisema kama Serikali itashindwa kufanya hivyo, chama hicho kitaitisha maandamano nchi nzima ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.
Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, kuwa anaweza kuifua CHADEMA kwa madai ya kusababisha vurugu, Bw. Mbowe alisema kuanzia sasa watafuata maagizo ya sekretari wa ofisi hiyo badala ya msajiri kwani kauli yake inahatarisha usalama wa nchi.
“CHADEMA si chama cha mfukoni bali kinaongozwa kwa misingi ya sheria na katiba, msajiri asifikiri chama hiki ni cha Mbowe, bali wanachama wake ni mamilioni hivyo akikifuta atawapeleka wapi.
“Kama anataka kukifuta ajaribu aone, kuanzia sasa hatutafanya kazi na Tendwa, ila tutafuata sheria na taratibu za ofisi yake hata kama maamuzi yatatolewa na sekretari,” alisema Bw. Mbowe.
Aliongeza kuwa, Bw. Tendwa kuanzia sasa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyonayo ambapo CHADEMA haitashiriki shughuli zozote ambazo ataziandaa lakini kama ataomba radhi kwa matamshi yake, wapo tayari kushirikiana naye.
Bw. Mbowe akizungumzia mgogoro uliokuwa jijini Mwanza na kusabnabisha Meya wa CHADEMA kuondolewa, alisema Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kupitia maelezo ya kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo, imeamua wawavua uanachama madiwani wao wawili ambao ni Bw Adam Chigulani (Kata ya Igoma) na Bw. Henry Matata (Kata ya Kitangiri).
“Hawa madiwani wamehusika na tukio hili hivyo kukikuka maazimio na misingi ya chama chetu, tupo tayari kwa lolote na wengine wataendelea kuchukuliwa hatua,” alisema.
Akizungumzia Operesheni Sangara, Bw. Mbowe alisema itaanza muda mfupi ujao kwani waliisimamisha baada ya mauaji ya watu wawili akiwemo marehemu Daudi Mwangosi (mwandishi wa Kituo cha Channel Ten), ili kutoa fursa ya chama hicho kuyajadili
source:majira
No comments:
Post a Comment