Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania tuna haki yakujivunia
amani tuliyo nayo kutokana na utawala bora uliodumishwa toka enzi za hayati
baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Rais wa Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar Bw Abeid Karume.Hali hii inajidhihirisha Maeneo mbalimbali
Nchini kutokana na amani na utulivu iliyotanda kutokana na uongozo madhubuti
unaojitahidi katika kuhakikisha amani na utulivu inatawala Nchini.
Taifa lolote bila yakuwa na amani lazima
kuwepo na machafuko ambayo yataigharimu Nchi kuingia kwenye machafuko ambayo
hayatasahaulika kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya utawala
bora(CEGODETA)Bw Thomas Ngawaiya anasema kuwa Tanzania ni moja katia ya Nchi
ambayo inapaswa kujivunia amani tuliyo ambayo imeanziswa na waasisi wa Taifa
hili.
Anasema Nchi kama Rwanda,Burundi,Somalia,Congo ni mifano halisi ya nchi
ambazo mzimejikita katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kutokuwa
na Uongozi imara.
Anaongeza kuwa Watanzania wanapaswa
kutambua kuwa Taifa lolote lisilokua na utawala bora ni sawa na gari lisilokuwa
na mafuta ambalo saa yeyote linaweza kuishia njiani.
Hata hivyo nasema kuwa Wananchi wanapswa kutoyumbishwa
na jamii au baadhi ya watu wanaotaka kuondoa amani ya Nchi yetu kwasababu zao
binafsi au itikadi zao binasi ili waonekane wao ndiyo bora.
Ngawaiya anasema kuwa utawala bora
haukubaliani nao na utahakikisha uatwala bora unahimarika na kudumishwa ili
Taifa letu liiisingie kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kama
zilivyo Nchi za jirani.
``Kwa kweli sisi kama
utwala bora hautuwezi kukubaliana na baadhi ya watu ambao kwa itikiadi zao
binfsi wamekuwa wakitaka kuivuruga amani ya Nchi yetu kwasababu zao
binfsi``anasema,Bw Ngawaiya.
Anasema kuwa migomo yoye iliyotokea hapa
Nchini chanzo chake kikubwa ni itikidai za watu binfsi ambao wantaka kuvuruga
amani ya Nchi yetu ili Serikali ione haijafanya jambo lolote kwa watu wake.
Bw Ngawaiya anasema kuwa watu kama hao utawala bora huatawafungia macho na utahakikisha
unawataja mara kwa mara ili wajirekebishe na kurejesha amani ya Nchi yetu
ambayo tumedumu nayo toka enzi za hayati Baba wa Taifa.
``Migomo yote inayotokea Nchini sisi kama
utawala bora tunayo vyanzo vyake ni baadhi ya watu wacchache ambao wanataka
Wananchi waichoke Serikali yao,ili waonekane wao wako juu,hivyo hatuo tayari
kulifumbia macho tatizo hilo na tutahakikisha tunawafichua ili wachukuliwe
hatua za kinidhamu``anasema,Bw Ngawaiya.
Aidha anasema kuwa madaktari pamoja na
waalimu wanapaswa kutambua kuwa kiapo walichoapa kipindi wanakuja kazini ni
kuhakikisha wanawatumikia Wananchi hivyo basi hawana budi kugoma.
``Nipende kusema katika Serikali yetu sekta
ambayo imepewa kipaumbele kuliko sekta zote ni sekta ya afya,hivyo basi
ninashangaa pale ninapoona wanagoma huku watanzania wakipoteza maisha tena kwa
kodi zao zilizotumika kuwasomesha``anasema,Bw Ngawaiya.
Anasema kuwa madaktari wamependelewa kwa
mambo mengi ikiwemo kupewa fedha wakati wakiwa kwenye mafunzo.pamoja na
nyongeza ya posho wakati wa muda wa nyongeza kazini.
Anasema kuwa hizo zote ni itikadi za baadhi
ya watu wachache ambao wanataka kuivuruga Serikali kwakutumia sekta muhimu ili
Serikali ionekane haijafanya kitu kwa wananchi.
``Kwa kweli tunalaani kwa vikali na kupinga
watu ambao wanataka kuipoteza amani ya Nchi kwa mambo yao binafsi,haya mambo tukiyanyamazia
yataligharimu Taifa letu ambaolo limedumu na amani tangu enzi za hayati baba wa
Taifa``anasema,Bw Ngawaiya.
Kwa mujibu wa Bw Ngawaiya anasema kuwa
watanzania,wafanyakazi wanatakiwa wasiyumbishwe na baadhi ya watu ambao kwa
itikiadi zao wanataka kuvuruga amani ya Nchi kwakuweka mapandikizi,chuki na
uzandiki ilimradi amnai ya Nchi yet itoweke.
Hata hivyo anasema kuwa Watanzania
wanapaswa kutambua yakuwa Nchi yetu ni moja kati ya Nchi ambayo inapaswa
kujivunia kwa amini pamoja na raslimali nyingi ikiwemo mbuga za wanyama,madini
madini ya Tanzanite. pamoja na madini ya
Tanzanite.
Bw Ngawaiya anasema kuwa kwanini tusijuvunie
na hizi raslimali tulizopewa na Mwenyenzi mungu,na badala yake tunajiingiza
kwenye migomo isiyo na tija hapa Nchini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
wafanyabishara wenye Viwanda,biashara pamoja na wakulima Mkoani Kilimanjaro (TCCIA)Bw
Patrick Boisafi anasema kuwa Viongozi wa Wananchi wanapswa kutambua utawala
bora siyo kutoa kauli bali ni kuhakikisha Viongozi wanashirikiana na Wananchi
katika kutoa maamuzi ili kuondoa migogoro isiyokuwa na ulazima.
Bw Boisafi anasema kuwa mgomo wa mabasi
uliotokea hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro ni moja katia ya ishara ambayo
inaashiria utawala bora unahitajika kusuluhisha ili yasitokee majanga kama hayo tena.
Hata hivyo anaongeza kuwa ipo haja ya
Serikali,wadau na taasisi mbalimbali Nchini kukaa chini na kuwafundisha
Wananchi juu ya utawala bora ili kuondoa migogoro baina ya Wananchi na Viongozi
wao.
Hata hivyo anasema kuwa Wananchi wanapaswa
kutambua yakuwa utawala bora siyo maisha bora kwa kila mtanzania kufanyiwa kila
kitu na Serikali bali utawala bora ni jinsi gani unavyoifanyia mambo ya maendeleo Nchi yako.
Aidha anasema kuwa Watanzania wanapswa
kufuta usemi wa maisha bora kwa kila mtanzania ni lazima Serikali ikufanyie
kila kitu,bali wanatakiwa kutumia fursa zilizopo kama mabenki,vyama vya akiba
na mikopo katika kukopa mikopo yenye riba nafuu ili iwakwamue kwenye hali ngumu
ya maisha.
``Maisha bora kwa kila Mtanzania siyo
lazima Serikali ikufanyie kila kitu,bali tunatakiwa tujibidiishe kwakufanya
kazi kwa bidii ili tumuondoe adu mbaya maskini ambaye amekuwa akituweka kwenye
hali ngumu ya maisha.
Anaongeza kuwa tatizo la Vijana walio wengi
hapa Nchini ni kushabikia vyama vya siasa pasipokuangalia mustalbali wa maisha
wa maisha yao
hali inayopelekea kuilaumu Serikali haijawanyia kitu.
``Maisha bora kwa kila mtanzania siyo
Serikali ikufanyie kila kitu,bali ni wewe mwenyewe unavyojituma na kutumia
fursa zilizopo kama mabenki,pamoja na vyama vya akiba na mikipo ili
vikunufaishe katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha``anasema,Bw Boisafi.
Bw Boisafi anasema kuwa Wananchi wanapswa
kutambua yakuwa maisha bora siyo mpaka Serikali ikuletee kila kitu mpaka nyumbani
kwako wewe mwenyewe badala yake wajikite katika kupambana na kazi ili iwe
suluhu ya matatizo yao.
Bw Boisafi anasema kuwa katika kuhakikisha
Wananchi wanajikomboa kwenye hali ngumu ya maisha,chama hicho kinawakaribisha
Wananchi wajiunge nacho ili wabadilishane ujuzi na uzoefu wa kibishara ili
waondokane na tatizo sugu la maisha.
``Tunawakaribisha Wananchi wote wanaotaka
kujiunga na chama chetu ili nao wanufaike na elimu yakujikwamue na tatizo sugu
la maisha linalowakabili watu wengi kwa sasa hapa Nchini.
Boisafi anawakaribisha watu wote
wanaohitaji kuja kuwekeza Mkoani hapa ili kuongeza ajira pamoja na kuwakwamua
watu kwenye hali ngumu ya maisha.
``Kwa kweli Kilimanjaro ni moja katia ya
Mji ambao tunajivunia una raslimali nyingi ikiwemo Mlima Kilimanjaro,mashamba
ya kahawa,hivyo basi kwa niaba ya Wanakilimanjaro tunawakaribisha wale
wanaotaka kuja kuwekeza waje ili tusukume gurudumu la maendeleo Mkoani
hapa``anasema,Bw Boisafi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment