Thursday, July 26, 2012

CWT KIMEANZA MCHAKATO WA KUSHINIKIZA MGOMO


CHAMA cha waalimu Tanzania(CWT) kimeanza mchakato wa upigaji kura kwa ajili ya kushinikiza mgomo wa walimu kutokana na tume ya usuluhishi kukipatia chama hicho cheti chakushindwa kusuluhisha mgogoro kati ya Serikali na Chama hicho.Hayo yalibainishwa, na Rais wa Chama hicho Bw Gratian Mukoba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Daresalaam jana juu ya kushindikana kwa mgogoro huo.

Alisema kuwa, julai 25 Chama hicho na Serikali walifika kwa msuluhishi ambaye ni Bw Cosmas Msigwa ambaye ameteuliwa na tume ya usuluhishi na uamuzi kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na hatimaye chama hicho kilipokea cheti chakushindikana kwa mgogoro hali ambayo imepelekea Wananchama kuingia katika mchakato wa upigaji kura.

``Zoezi la upigaji kura limeanza, toka jana na linaendelea mpaka kesho saa tatu,ambapo kura zitapigwa mchana na usiku ambapo kupitia kura hizo zitatoa maamuzi ya Wananchama kuwa na mgomo au laa``alisema,Bw Mukoba.

Hata hivyo alisema kuwa, mgogoro huo unahusu maslahi ya Waalimu ikiwemo ongezeko la kima cha chini cha mishahara lakini chama hicho kinashangazwa na tamko la Serikali kuitaka CWT kuwakilisha takwimu za waalimu wanaopaswa kulipwa ili ifanye hesabu kwani hawajui ni waalimu wangapi wanastahili kulipa na huenda wengine wameshakufa huku pia ikisema kuwa haina uwezo kiuchumi wa kuongeza posho hizo


Bw Mukoba alisema, hoja hiyo ni yakupotosha ukweli wa madai ya waalimu kwani Serikali ina takwimu za matumizi ya zaidi ya trilioni nne kwa ajili ya kulipa mishahara ya waalimu kwa viwango.

Kwa Upande wake kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw Ezekiah Oluoch alisema, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza aina ya mgomo na muda utakaotumika sambamba na kutoa notisi ya saa 48 kwa Katibu Mkuu Kiongozi alinde mali zake.

Aliwataka Wananchama wa Chama hicho kuunga mkono ongezeko, la mishahara asilimia 100,posho yakufundishia waalimu wa sayansi kwa asilimia 55,waalimu wa sanaa asilimia 50 pamoja na posho ya mazingira magumu kwa asilimia 30 huku wakiwaomba wanafunzi na wazazi watakaoathirika na mgomo huo kuwavumilia waalimu.






No comments:

Post a Comment