Thursday, July 26, 2012
KNCU BIMA YA AFYA IKO JUU KWA WAKULIMA WA KAHAWA
WANANCHI wa Kata ya Okaoni Kijiji cha Oria iliyopo Wilayani Moshi Vijijini wamelalamikia Chama cha Msingi(KNCU)kwakuwatoza Wakulima wa zao la kahawa kiasi cha shilingi elfu ishirini na tano hadi thelathini na tano kwaaajili ya huduma ya kujiunga na bima ya afya jambo ambalo wamelipinga Wananchi hao kutokana na gharama hizo kuwa kubwa ikilinganisha hali ya kipato chao.
Akizungumza kwa niaba ya Wakulima wenzake niaba ya Wakulima wenzake kwenye mkutano wa maendeleo ya Kijiji hicho Bi Francis Tamamu alisema kuwa, kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaokuja kudai kiasi hicho kwa kigezo cha huduma za afya jambo ambalo wameona ni wizi. Alisema kuwa, kumekuwa na watu wanaopita majumbani mwa watu kuwahimiza wachangie huduma hiyo kwa haraka ili waweze kutimiza malengo yao yakuchangisha kiasi hicho.
Alisema kuwa, wamekuwa wakitozwa kiasi cha shilingi elfu ishirini na tano hadi thelathini kwa kila kaya jambo ambalo wameona ni gharama kubwa ukilinganisha gharama zilizowekwa na Serikali. Aidha aliomba fedha zilizokusanywa, chama cha ushirika(KNCU)zirudishwe ili waweze kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF)kutokana na unafuu uliopo katika Mfuko huo.
Kwa upande wake ani wa Kata hiyo Bw Moris Makoi alisema kuwa kitendo kilichofanywa na chama cha ushirika(KNCU) cha kwenda kwenye kaya za Wananchi na kukusanya kiasi hicho ni kitend cha wizi amabacho hakiwezi kuvumiliwa. Aliongeza kuwa, Serikali imeshatoa maelekezo kupitia Halmashauri kiwango cha kujiunga na bima ya afya ni shilingi elfu kumi kwa kila kaya ambapo unatibiwa familia yako na mwenzi wako nakuongeza imekuwa ikikusanya kiasi cha shilingi elfu thelathini na tano kwa kila mtu mmoja.
Hata alisema kuwa, itakuwa ni vigumu kwa Wananchi maskini kama hao kuzimudu gharama hizo nakuongeza kuwa KNCU ingekuja na mpango mkakati wakuelimisha Wananchi juu ya kilimo cha zao la kahawa badala yakujiingiza kwenye mambo ya afya. Aidha alisema kuwa, KNCU inatakiwa ijikite kwenye masuala ya kuwaelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa zao kufufua za la kahawa kuliko kujikita kwenye mambo ya afya ambayo hawajajipanga.
Bw Makoi alisema kuwa, Halmashauri hiyo inaendelea na taratibu zakuwaelimisha Wananchi kujiunga na bima ya afya kwa shilingi elfu kumi badala ya shilingi elfu thelathini na tano zinazotozwa na KNCU huku akimtaka Waziri wa Kilimo chakula na ushirika aingilie kati jambo hilo la KCU lakuwatoza Wananchi maskini nakuchukua fedha zao nyingi kwaajili yakuwaahidi huduma ya afya.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment