Thursday, June 21, 2012

UNYANYASAJI BADO NI TATIZO

Ofisi ya Dawati la Wanawake katika Kituo cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam wamesema matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa wilaya hiyo yaliyoripoti kwa mwaka huu yamefikia 23.


Akizungumza na chombo cha habari jijini Bi. Jeni Fred Chila ambaye ni msimamizi wa dawati hilo jana, jijini Dar es Salaam, alisema kuwa idadi ya makosa imeongezeka ukilinganisha na ya mwaka jana.

"Kesi zote ambazo tumezipokea ni za vitisho na ulawiti,"alisema.

Bi.Jeni alisema kuwa watu wengi wanahitaji elimu kuhusu dawati hilo na wajue kuwa lipo dawati la wanawake linayoshughulikia masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na hata wanaume wanaonyanyaswa nao watoe taarifa kwao.

Hata hivyo alitoa mwito kwa jamii itoe elimu kwa watoto ambao wanatendewa vitendo vya kinyama na ukatili mara kwa amara.

Baadhi ya makosa yalioripotiwa ni kumshika mwanamke bila ridhaa, kujaribu kulawiti, kulawiti mfanyakazi wa ndani, kubaka, usafirishaji haramu kwa binadamu, vitisho vya maneno pamoja na vitisho kimwili.

Aliongeza kuwa, kwa sasa wamejipanga kuwasaidia watu wote ambao wananyanayswa ili kuwapatia msaada.

No comments:

Post a Comment