Wakazi wa Tabata Segerea wameingia kwenye mgogoro na mwekezaji wa kiwanda kinachojihusisha na upasuaji wa magogo L-Line corporation (T) LTD
Mgogoro huo unadaiwa kusababishwa na umiliki mwekezaji huyo kutokana na wananchi kudai kuwa kiwanda hicho kina athari kwa wananchi.
Mwekezaji wa kiwanda hicho Bw.Kim Kyun ambaye ni raia wa Korea, alipoulizwa kuhusiana na malalamiko hayo, alidai ana uhalali wa kumiliki eneo hilo kwani taratibu zote zilifuatwa kwa ajili ya kuanzisha kiwanda hicho
Alisema kiwanda hicho hakina madhara kwa binadamu, kwani wanatumia mashine za kisasa, ambazo hazipigi kelele wala kutoa vumbi ambalo linaweza kudhuhuru wananchi.
Mmiliki huyo alisema awali kiwanda hicho kilikuwa Buguruni kwenye jengo la Sukita,kabla ya kuhamishiwa Tabata Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Bw. Samuel Binagi, alisema kuwa ana taarifa ya kuwepo kwa kiwanda hicho na alitoa ushauri kuwa wafuate utaratibu wa kumiliki eneo hilo.
Aliongezea kuwa kutokana na malalamiko ya wananchi alipeleka taalifa hiyo kwa halmashauri ya manispaa ya Ilala nao walitoa notisi ya kubomoa jengo hilo na kusimamisha ujenzi na biashara hiyo
No comments:
Post a Comment