*adai kupokea uponyaji
Prof. Mwandosya aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana baada ya muda mrefu kutoonekana katika vikao vya Bunge mjini hapa kwa sababu ya kuumwa na kwenda kutibiwa nchini India.
Muda mfupi kabla Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, hajaanza kusoma hotuba yake, Prof. Mwandosya aliingia ndani ya ukumbi huo akiwa na afya njema na kusaababisha wabunge kumshangilia kwa makofi.
Jambo hilo lilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Bi. Jenista Mhagama, kumwambia Dkt. Mwakyembe asimame kusoma hotuba yake kwa muda ili aweze kutoa fursa kwa bunge kueleza nini kilichopo
mbele ya wabunge hao.
Bi. Mhagama aliwaambia wabunge kuwa, shangwe hizo zilitokana na kurejea kwa Prof. Mwandosya bungeni na kudai huo ni muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu.
Baada ya muda kidogo, Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, alitoa hoja ya kutaka Prof. Mwandosya apewe muda wa kusema kidogo ndani ya Bunge na kuungwa mkono.
Bi. Mhagama alikubali hoja hiyo na kuridhia ombi la Bw. Sitta kwa mujibu wa kanuni namba 5(1), hivyo alimruhusu Prof. Mwandosya kwenda mbele ili kuzungumza machache.
“Naomba nitoe shukurani zangu kutoka moyoni kwa Watanzania wote, kumbe ukiugua hakuna chama CCM, CHADEMA wala TLP ambacho kitashindwa kukutafuta na kukuombea, wote wanakuombea na kukuona ni Mtanzania wa kawaida.
“Nawashukuru Watanzania wote hasa sana Rais Jakaya Kikwete ambaye alisisitiza sana afya yangu ni jambo muhimu sana, alinitaka niondoke nchini na kwenda kutibiwa nje,” alisema.
Aliongeza kuwa, wakati anaumwa Rais Kikwete alipokwenda kumuona, alimtaka asiwe na mawazo ya kutatua kero za wananchi wake kama maji bali ahangaikie afya yake ambayo ni muhimu.
Alitoa ushauri kwa wabunge wenzake kupima afya zao kwani yeye kwa miaka 45, hakuwahi kulala kwenye kitanda cha hospitali bali ameanza kukitumia Hyderabad Apollo, nchini India.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zito Kabwe (CHADEMA), alipewa nafasi kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kutoa neno la shukrani hivyo alimshukuru Mungu kwa kumpa afya njema Prof. Mwandosya na kuahidi kuwa, kambi hilo itaendelea kumpa ushirikiano mkubwa.
No comments:
Post a Comment