Thursday, August 9, 2012
KUTENGANA KWA WAZAZI KUMESABABISHA KUPOOZA MWILI
TANZANIA ni miongoni mwa nchi zilizokuwa ndani ya jumui ya Afika Mashariki ambayo inajulikana kama kisiwa cha amani kutoka na viongozi wake kujitahidi kudumisha amani na upendo kwa wananchi wake . Kutokana na sifa hiyo imefanikiwa kuheshimiwa na nchi mbalimbali ndani na nje ya jumuia hiyo,nah ii inatokana na kuwepo kwa viongozi ambao wamekuwa wakijitahidi kuakikisha amani inakuwepo.
Lakini kuepo kwa sifa hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la ongezeko la watoto wanaozagaa mitaani kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa kwa upendo kutoka kwa wazazi ama walezi wao Asilimia kubwa ya watoto wanaozagaa mitaani na kujingiza kwenye makundi maovu hutokana na kukosa malezi bora na wengine hukimbia kunyanyaswa mara baada ya wazazi wao kufa ama kutengana.
Kutokana na sababu hiyo inapelekea watoto kuzikimbia familia zao na kusababisha kuishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa maisha yao, hivyo ili wajikwamue wanajikuta wakishawishika kuingia katika makundi yasiyoendana na umri wao.
Makundi hayo ni pamoja na biashara ya kuuza miili yao ambapo ukitembelea sehemu ambazo biashara inafanyanyika lazima utakutana nao wakiwa wamejichanganya na na watu wazima wakisubiri wateja.
Kutokana na kujingiza katika biashara hiyo wanajikuta wakipatwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuambukuzwa magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI na mimba za utotoni.
Kati ya watoto ambao wamekumbana na mikasa ya kuterekezwa na wazazi wao akiwemo Bi. Domina Beatus (17) mkazi wa Mwanza ambaye kwa sasa anaishi Dar es Salaam
Mtoto Beatus anasema alitoroka nyumbani kwao akiwa na miaka (12) baada ya kukosa mazingira rafiki kutoka kwa wazazi wake baada ya mama yake kutengana na baba yake hali iliyopelekea aishi geto(danguro)
“Niliacha shule nikiwa darasa la tano na kuyakimbia mazingira ya nyumbani kutokana na manyanyaso mbalimbali ikiwemo kufanyishwa kazi za ndani bila ya kupumzika kufua nguo za ndani za mama “ anasema
Anasema kwa sababu hiyo aliamua kutoroka nyumbani na kwenda kijiji cha pili kinachoitwa Miti Mirefu mkoani Mwanza na kuishi geto na kujiingiza katika makundi yasiyo faa ikiwemo kujiuza pamoja na kutumia madawa ya kulevya
“Nilitoroka kwenda kikiji cha pili cha Miti Mrefu na kuanza kujiuza kwa wanaume tofautitofauti ili nipate kipato kwa ajili ya kujikimu kimaisha lakini kwa kuwa nilikuwa na wenzangu wanaotumia dawa za kulevya nikashawishika na mimi kuzitumia pamoja na kunywa pombe gongo, na kutafuna mirungi, “ anasema
“Nilikuwa na uwezo wa kulala na wanaume watano hadi sita kwa siku na walikuwa wananilipa sh.30000 kama ni mtu mzima lakini kijana mdogo sh. 15000, wanaume wengi nilio kuwa nalala nao walikuwa hawataki tutumie kinga kwa sababu ya madai kuwa wanakosa radha “ anasema
Anaendelea kusimulia kuwa baada ya miaka mitatu kukaa mkoani hapo huku akiwa akiendelea na biashara hiyo ndipo alipokutana na dalalali wa wafanyakazi wa ndani ambaye hata jina lake hakulijua na kuwashawishi kuja Dar es Salaam kufanya kazi za ndani kwa mshahara wa sh. 40,000
Anasema kwamba walichokidhania hakikufanikiwa kwani walifika jijini usiku na hawakumpata mwenyeji wao hivyo walilazimika kutafuta wanaume wa kujiuza ili waweze kupata hela ya kula na hifadhi ya usiku ule na ndipo asubuhi alipokuja mwenyeji wao kuwapokea(mwajiri wao)
Anasema baada ya kukutana na mwajiri wake alijulikana kwa jina moja Bw. Nyaule mkazi wa Kitunda alianza kazi za ndani rasmi kwa mategemeo kuwa shida zake na malengo yake yatafanikiwa na kusahau shida alizokumbana nazo kipindi cha nyuma
Lakini hali haikuwa hivyo kwani alijikuta akifanyishwa kazi za ndani bila ya kulipwa kama walivyokubaliana badala yake akijikuta akitongozwa na mwajiri wake na kumdanganya kuwa atamuoa na kumuacha mke wake
“Niliendelea kunyanyasika kama nilivyozoea kwani nililazimika kufanya kazi bila kulipwa mshahara kwa muda wa miezi 7 na huku bosi wangu akiwa ananitaka kimapenzi huku akinidanganya kunioa na ikiwezekana kumuacha mke wake” anasema
Anasema baada ya hali hiyo aliona ni vyema kumtaalifu mke wake ili amkanye mumewake lakini kitendo hiko kilisababisha mwajiri huyo kumfukuza kwa madai kuwa anawagombanisha na mke wake
Anasema baada ya hapo akanza maisha ya kutangatanga katika kujitafutia mahitaji muhimu hali iliyopelekea kukutana na mwanaume mwingine anayeitwa Baraka na kuanza naye mahusiano na kuishi pamoja kama mke na mume kwa wazazi wa huyo mwanaume
Anaendelea kuhadithia siku moja mama mkwe wake(mama yake Baraka)alimuuliza kuhusu swala zima la kuzaa kuwa katika kipindi alichokuwa akiishi pale hajaweza kupata mtoto,kutokana na hali hiyo akachukua uamuzi wa kwenda kwa watu wanaombea ili aweze kupata mtoto
“Ustahdi alishindwa kuniomboa kwa lengo hilo na kunishauri kuwa atanisaidia kuniombea ili nirudi nyumbani kwakuwa umri wangu ulikuwa mdogo ,zoezi hilo halikufanikiwa kwa kuwa lengo langu mimi ni kupata mtoto.”anasema
Anasema baada ya muda mfupi akapatwa na mtihani wa kupooza baadhi ya viungo kuanzia kiunoni mpaka miguuni nakupelekwa hospitali za watu binasfi kwa ajili ya matatibabu lakini hakupata nafuu ndipo walipoamua kumpelekea kwenye maombi katika kanisa la Saa ya Ufufu na Uzima lililopo Kawe jijini Dar es Salaam
“Baada ya kupooza walinipeleka kanisani kwa muombezi lakini cha kushangaza waliniterekeza kanisani hapo ambapo maisha yangu yalikuwa ni kulala njee kula kwangu kwa kuombaomba kwa waumini wanaokuja hapo kanisani “ anasema
Anasema alikaa kanisani kwa muda wa miezi 9 bila ya mafanikio yoyote alibaki katika hali ile ile ya kutambaa na kuburuzika huku viungo vikiwa havina nguvu ya kusimama
Alipouulizwa mchungaji wa kanisa hilo la Saa ya Ufufuo na Uzima Bw. Joseph Marwa alisema kuwa ni kweli binti huyo alikuwepo kanisani hapo kwa muda huo wa miezi 9, na walijitahidi kumpa huduma ya kiroho
Alisema kuwa kanisani hapo kazi yake ni kutoa mafundisho na kutoa mapepo na si kutoa huduma ya malazi hivyo walimsaidia mtoto huyo katika huduma hizo na si kumpatia malazi
“Hapa kanisani hakuna nyumba za kulala aliweza kupata msaada wa chakula kwa waumini wa hapa hivyo tuliweza kumuombea lakini cha kushangaza alikuwa haponi,ingawa alikili kuokoka”alisema mchungaji Marwa
Marwa aliongezea kuwa aliweza kuishi hapo kanisani akiwa anapata msaada pamoja na kufuliwa nguo zake na kuogeshwa na waumini wa hapo lakini cha kushangaza watu wanaodai kuwa ni ndugu zake pamoja na mume wake walikuja kumchukua kanisani hapo
Mtoto Domina aliendelea kusimulia kuwa baada ya kukaa hapo kanisani kwa muda huo hatimaye wale waliomterekeza walikuja kumchukua tena na kumpeleka nyumbani akiwa yuko vilevile hawezi kutembea na ndipo dada yake Baraka kuamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu
Akizungumza na Majira dada yake Baraka (wifi yake domina) Bi. Easter Peter alisema kuwa aliamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji kutokana na hali yake kuwa mbaya kwani alishazunguka kila sehemu lakini hakupata nafuu yoyote
Alisema aliamuwa kubeba juku hilo kwani hakuona sababu ya kumterekeza kwani alikuwa akihitaji msaada wa kupona ili aweze kuendelea na maisha yake kama awali niliamini nikimpeleka kwa mganga huyo ataweza kupona kwani alishawaponeshwa watu wenye tatizo kama la mtoto huyo
Akizungumza na gazeti hili mganga huyo Bw. Abubakhari Shabani ‘Komboleza’mkazi wa Chanika alisema kuwa alimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya ya kutoweza kutembea wala kwenda kujisaidia mwenyewe
Bw. Komboleza alisema kuwa aliweza kujitahidi kumtibu kwa miezi mitatu mtoto huyo na sasa anaweza kusimama mwenye kwa kutumia msaada wa fimbo jambo ambalo hapo awali alikuwa hawezi
Komboleza anaongezea kuwa kwa kipindi chote hicho mtoto huyo anaishi kwake na wale waliompeleka wamemterekeza hivyo hapati msaada wowote ule kutoka kwa mtu yoyoteyule
“Wameletwa hapa kwangu na kumterekeza akiwa hawezi kutembea wala kusimama nimempa tiba kwa gharama zangu binafsi pamoja na chakula kwa kipindi chote hicho kwani niliona anahitaji kupewa msaada ingawa na mimi sasa nimeshindwa kuendelea kutoa msaada huo” anasema Komboleza
Kwa upande wake mtoto Domina anasema kuwa kulingana na hali yake kuwa nzuri kidogo kwa sasa anaomba msaada wa nauli kwa ajili ya kurudi kwao Mwanza
Anasema kuwa maisha aliyoyapitia ni magumu kwa kipindi chote cha miaka 5 kwake imekuwa ni fundisho na kuamini kuwa kukimbia nyumbani si kutatua tatizo bali ni kiuongeza tatizo kubwa
Mtoto huyu anayesumbuliwa na kupooza baadhi ya viuongo anaomba msaada kwa wasamalia wema wa nauli kwa ajili ya kurudi nyumbani kwao mkoa wa Mwanza , kwa yeyote Yule aliyeguswa na mtoto huyo anaweza kuwasiliana na namba 0657112952 ili kuwakilisha msaada wa nauli
Labels:
Tuwajali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment