Friday, July 13, 2012
WACHAGA KWA KITOCHI!
Mpenzi msomaji karibu katika safu yetu ya utani wa Jadi, tulitembelewa na mtu kutoka Upareni ambaye yeye aklisema kuwa Kitochi ni muhimu kwa wachaga ambao hutumika katika makutano ya ndugu jamaa kwa ajili ya kuburudika kwani lazima kiwepo kwani bila hivyo huwezi kumpata mtu katika mkutano huo au kikao chochote kile.
Alielezea kuwa kitochi ni kipimo cha pombe ambacho kinaujazo wa nusu lita ,mara nyingi kitochi hutumika wakati pale mtu anapokusanya wazee ili kuzungumza nao swala Fulani au mtu analeta posa na anataka ijadiliwe na wazee au katika mashauri mbalimbali yanayokutanisha wazee
Anaongezea kuwa hata wanapokuwa mbali yaani mkoa mwingine hutumia mbege au bia kukusanya wazee na wanafanya kikao sehemu moja na mambo yanakwenda kama yalivyopangwa,mbali na hilo pia ukirudi nyumbani yaani kama unaishi mkoa mwingine na umeamua kurudi nyumbani unapopokelewa na wazee lazima watatumiam lugha ya kukuomba ‘kitochi ‘ baada ya kukupa pole ya safari neon kitochi ndi linafwata hii ni kuikamilisha mila yao na utamaduni wa kwao
Je makabila mengine kama wanyamwezi, Wahaya, Wakurya, Wajita, Warundi, Wasukuma, Wahehe, na makabila mengine wanatumia utaratibu gani??????
Kama unautani wa kabila lolote ule tutumie katika (gviews08@gmail.com)
Labels:
Utani wa Jadi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment