Sunday, July 15, 2012

DROGBA ATUA SHANGHAI-ASISITIZA KWENDA KWAKE SIO KWA AJILI YA PESA




Mjini Shanghai mamia wa mashabiki wa soka mjini Shangai walijitokeza kumpokea huku wakishangilia mchezaji wa kimataifa na raia wa Ivory cost Didier Drogba.

Mwanasoka huyo alifanya mechi yake ya kwanza rasmi na timu mpya mchana huo Shanghai Shenhua Jumamosi na alisisitiza hoja yake ilikuwa motisha kwa changamoto ya kusaidia soka ya Kichina .

alinukuliwa akisema"Sikuja hapa na wazo la kutengeneza fedha nyingi," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 katika mkutano wa waandishi wa habari, licha ya taarifa za zilizoenezwa na vyombo vya habari za kuonesha kuwa yeye ni mchezaji anayeongoza kwa kulipwa zaidi ya USD 300,000 kwa wiki.

"Nimekuja hapa kwa sababu ya changamoto tofauti kabisa na niliwahi kukutana nazo pindi nikiwa Ulaya," alisema.

"Mimi niko hapa na kushinda mechi na kuwa bingwa - mimi sipo hapa kwa ajili ya kustaafu," aliongeza.

Muda mfupi baada ya kufunga penalti ambayo iliipa Chelsea taji la mabingwa wa Ulaya, Drogba alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu na Shenhua. Kwa namna hiyo Drogba anaungana na mchezaji wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka - ambaye anachezea klabu aliyojiunga nayo.

"Tuna kazi ngumu ya kufanya, lakini tutafanya kazi kwa bidii na kujaribu kufanya mashabiki wetu waweze kufurahi," alisema Drogba, “Labda inaweza kuchukua muda kuifikisha china kwenye mafanikio, lakini tutafanya kila linalowezekana kufikia mafanikio."

Kuwasili kwake inafufua matumaini mapya kwa vilabu vya soka nchini china na matumaini ya kupanda kwa viwango vya uchezaji wa wanasoka wa kichina. Wafuasi wa soka nchini china wanasema kuwa wachezaji wa kichina watajifunza soka bora kutoka kwa nyota bora ya kimataifa na kufanya soka la china kuwa lenye kiwango cha kimataifa.

Hata hivyo, wakosoaji wameeleza kuwa kununua wachezaji toka ulaya kuendeleza soka china sio jawabu la kukuza soka nchini china.wakosoaji hao waliendelea kusema kuwa Mmiliki wa Shenhua Zhu Juni angeliweza kuwekeza kwenye soka la vijana kama nia yake ni kukuza soka lachina na sio biashara zake. Hata hivyo kutua kwa Drogba kwenye timu hiyo kumekuwa kama baraka baada ya timu aliyojiunga nayo kuifunga mpinzani wake mkubwa Beijing Guo mabao 3 kwa 1 katika mchezo wake wa nyumbani uliochezwa jumamosi.

No comments:

Post a Comment